Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Mji
Kibaha mkoani Pwani (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi
yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma mkoani humo.
Baadhi
ya Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani
wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani)
alipokuwa akizungumza nao kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo
wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa
watumishi hao.
Afisa
Misitu wa Halmashauri ya Mji Kibaha mkoani Pwani, Bw. William Msemo
akiwasilisha hoja ya kiutumishi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kwenye ukumbi wa
Halmashauri ya Mji huo wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la
kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao.
Walengwa
wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wa Kitongoji cha Mwanabwito,
Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake
ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya TASAF mkoani Pwani.
Mbunge
wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa neno la shukrani
kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipofanya ziara ya kikazi yenye
lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma Wilayani Chalinze.
Mbunge
wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Mhe. Michael Mwakamo akitoa neno la
shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipofanya ziara ya
kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma na
kukagua miradi ya TASAF wilayani Kibaha.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkuu wa TASAF, Bw. Paul Kijazi akitoa maelezo kwa Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Deogratius Ndejembi kuhusu mradi wa jengo la kitega uchumi la
kikundi cha Wazee wa Mlandizi lililojengwa na TASAF.
Kikundi
cha Wazee wa Mlandizi kilichonufaika na mradi wa jengo la kitega uchumi
lililojengwa na TASAF wakiwa mbele ya jengo hilo.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka Watumishi wa Umma nchini kulipa deni
kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mhe. Samia Suluhu Hassan
kwa kutoa huduma bora kwa wananchi na kutumia weledi wao kujenga uchumi
wa taifa.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na watumishi wa
Halmashauri ya Mji Kibaha, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha na
Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani, Mhe. Ndejembi amesema
kuwa Mhe. Rais alipoingia madarakani, alitoa maelekezo kwa Waajiri wote
kuzingatia maslahi ya watumishi wa umma hususani suala la upandishwaji
wa madaraja jambo ambalo hivi sasa limetekelezwa na linaendelea
kutekelezwa na waajiri wote kikamilifu ikiwa ni pamoja na kulipa stahili
za watumishi kwa wakati.
Amesema waajiri wote nchini
wametekeleza maelekezo ya Mhe. Rais, hivyo Watumishi wa Umma hawana budi
kufanya kazi kwa bidii na uadilifu kwani hakuna haki isiyokuwa na
wajibu.
“Ni muda mrefu tumekuwa tukililia haki ya kupandishwa
madaraja na kupewa stahili nyingine, Rais wetu ametusikia kwani wote
waliostahili kupanda madaraja, wamepanda na wenye madai ya stahili zao
mbalimbali wamepatiwa, hivyo hili ni deni na ili kulilipa deni hili
tunapaswa kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii na uadilifu,” Mhe.
Ndejembi amesisitiza.
Ameongeza kuwa, Serikali itaendelea kujali
maslahi ya Watumishi wa Umma kwasababu watumishi ndio injini ya
Serikali, hivyo wanalazimika kuendelea kutekeleza wajibu wao ipasavyo.
Aidha,
Mhe. Ndejembi amezungumzia changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika
zoezi la upandishwaji wa madaraja kwa Watumishi wa Umma kutokana na
baadhi yao kukosa sifa kwa kutojaza Fomu ya Mfumo wa Wazi wa Mapitio na
Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS).
“Changamoto ya upandishwaji
madaraja kwa baadhi ya Watumishi ni kupuuza ujazaji wa OPRAS, hawajazi
kwa wakati na wanajaza kwasababu wanaona ni kigezo tu cha upandaji wa
madaraja.” Mhe. Ndejembi amefanua.
Ili kuongeza ufanisi
kiutendaji, Mhe. Ndejembi amewahimiza Watumishi wa umma nchini kufanya
kazi kwa ushirikiano ili kufanikisha lengo la Serikali la kutoa huduma
bora kwa wananchi.
Katika hatua nyingine Mhe. Ndejembi amewataka
Watumishi wa Umma kushiriki katika kutoa elimu kwa walengwa wa Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini wanaonufaika na Mradi wa kutoa ajira za muda.
Amesema
suala la usimamizi wa walengwa wa TASAF ni la watumishi wote, hivyo ni
vema watumishi wenye utalaam katika fani mbalimbali wakatoa elimu ya
kuwawezesha walengwa kutimiza malengo yao badala ya kuwaachia Waratibu
wa TASAF pekee.
Aidha, amewataka walengwa wa TASAF kutumia vizuri
ruzuku wanayoipata kujikwamua katika lindi la umaskini ili hapo baadae
waache kutegemea ruzuku ya TASAF.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo
la Chalinze, Mhe. Ridhiwan Kikwete amesema kilio kikubwa cha Watumishi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kilikuwa ni suala la upandishwaji
wa madaraja jambo ambalo limetekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita.
“Mhe.
Naibu Waziri tunashukuru sana kwa kututembelea, changamoto kubwa
iliyokuwa ikitusumbua ni upandishwaji wa madaraja, suala ambalo
limeshafanyiwa kazi, tunamshukuru Mhe. Rais kwa kuliona hili na
kulitekeleza.” Mhe. Ridhiwan ameongeza.
Mhe. Ndejembi amefanya
ziara ya kikazi katika halmashauri hizo kwa lengo la kuhimiza
uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma, kukagua utekelezaji wa miradi ya
TASAF, ikiwa ni pamoja na kujiridhisha na utekelezaji wa maelekezo ya
Mhe. Rais ya upandishwaji wa madaraja kwa Watumishi wa Umma nchini.
Post A Comment: