Na Woinde Shizza , ARUSHA
Baadhi
ya wananchi wa Jiji la Arusha wamewalalanikia wasomaji mita za maji wa
mamlaka ya maji Safi na maji taka Arusha (AUWASA ) kuwazidishia bili za
maji pindi wanapokwenda majumbani
Waliyasema
hayo juzi wakati walipokuwa wakiandamana kuelekea Katika ofisi za
mamlaka hiyo ambapo walisema kuwa julio chao kikubwa kulichowafanya
waandamane ni kwenda kulalamikia tatizo la bili kuletewa bili kubwa za
maji za maji tofauti na matumizi yao.
Akiongea
na waandishi wa habari Moja wa wananchi hao Joseph John Mkazi wa mbauda
Jr alisema kuwa wasomaji mita ndio tatizo tatizo kubwa kwani wamekuwa
wanasoma mita lakini wanavyoenda kupiga mahesabu wanatuma majibu tofauti
na walivyosoma mita.
"Mfano
mimi walivyokuja kunisomea mita ilikuwa inasoma nimetumia unit 26
lakini walipoenda uko ofisini kwao wamenitumia bili inayoonyesha
nimetumia unit 47 kitu ambacho sio cha kweli mimi nimezoea kulipa bili
elfu 9000 Sasa wanavyoniletea bili ya efu 44000 kwa mwezi wanategemea
nini mimi nalipaje "alibainisha John
Alibainisha
kuwa alipofika idara ya maji kutoa malalamiko walimsikiliza
nakumwambia hilo ni tatizo la kibinadamu na watalifanyia kazi na
atarudia kulipa bili Kama awali alivyokuwa analipa.
Alitoa
wito kwa uongozi wa AUWSA kuwapa elimu ya kutosha wasomaji mita kwani
kwa asilimia kubwa wanaonekana awana elimu ya kutosha,huku aliwataka
kuhakikisha wanapokwenda kusoma mita wahakikishe wapo na mwenyeji
ambaye atahakikisha jinsi walivyosoma na kuandika ni ukweli ili
malalamiko yapungue
Neema
Raphael mkazi wa moshono aliwataka AUWSA kutoa elimu kwa wananchi juu
ya elimu ya usomaji mita pia aliwataka wasome bili kwa usahihi na pia
kuwepo na ushirikishwaji baina ya wafanyakazi wa mamlaka ya maji na
wananchi.
Akiongelea
swala hilo mkuu wa kitengo na mahusiano ya umma kutoka mamlaka ya maji
Safi na maji taka (AUWSA) Masoud Katiba alisema kuwa amepokea
malalamiko hayo lakini sio ya kweli kwani wao kama AUWSA wamekuwa
wakiwashirikisha wateja wao usomaji mita na Kama wengine wakiwakuta
hawapo wamekuwa waki tumiwa bili zao kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu
(sms).
Alisema kuwa swala
la kuzidishiwa wa bili linatokana na matumizi ya mteja jinsi
anavyotumia maji ndivyo jinsi anavyoletewa bili inavyokuja ,pia alisema
kuwa bili kuwa kubwa kunatokana na mambo mbalimbali ikiwemo kuvuja kwa
bomba upande wa mteja yaani mbele ya mita .
Alisema
kuwa wametenga dawati la huduma kwa wateja linaloshulikia kero kwa
ajili ya wateja wao ambapo mbali na hilo dawati hilo limekuwa kutembelea
wateja wao kwa ajili ya kukagua miundombinu ya maji ya wateja.
Post A Comment: