Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (kulia) akiangalia moja ya mbegu za malisho aina ya Juncao zinazozalishwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 28- Julai13, 2021.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Wadau wa Uvuvi kuhusu Samaki aina ya Kambakochi alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 28- Julai13, 2021. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel akimuangalia kuku wa mapambo kutoka Malaysia ambaye bei ya kumnunua ni Shilingi Laki Saba na Nusu. Prof. Ole Gabriel alimkuta kuku huyo katika moja ya mabanda ya Wadau wa Mifugo waliopo katika Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 28- Julai 13, 2021.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (kulia) akielekeza jambo kwa Maafisa wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) kuhusu machinjio ya Samaki aina ya Jodari alipotembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 28 - Julai 13, 2021.
Na Mbaraka Kambona,
Naibu Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewahimiza vijana kuchangamkia fursa
zilizopo katika Sekta za Mifugo na Uvuvi ili waweze kuzitumia
kujikwamua kimaisha.
Ulega alisema hayo alipotembelea banda la
Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya
Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere
jijini Dar es Salaam Julai 5, 2021.
Akiwa katika maonesho hayo
alisema kuwa vijana waitumie nafasi hiyo ya maonesho kwenda kujifunza
fursa mbalimbali za kibiashara na za uwekezaji zinazopatikana katika
sekta za mifugo na Uvuvi kwani Wizara ya Mifugo na Uvuvi mambo yake
mengi ni ya uzalishaji na biashara.
"Kila kitu Kilichopo katika
Wizara hii ni fursa katika Biashara na ni fursa ya uwekezaji, hivyo
tunawashauri vijana kutumia fursa hii ya maonesho kujifunza na kutumia
elimu watakayoipata kuboresha maisha yao huko wanakoishi," alisema Ulega
Aliendelea
kusema kuwa katika banda la Wizara hiyo kuna Wataalam mbalimbali ambao
wanatoa elimu na mafunzo yanayohusu ufugaji, hivyo wakifika hapo
watajifunza namna ya kufuga kuku, ng'ombe, mbuzi au Samaki kibiashara.
Aliongeza
kuwa kuna vijana wengi wanaotafuta kazi lakini bado hawajafanikiwa,
hivyo aliwashauri kwenda kujifunza fursa kubwa za kibiashara
zitakazowasaidia kujipatia ajira na kukuza uchumi wa nchi pia.
"Serikali
ya awamu ya sita ya Mhe. Samia Suluhu Hassan imejikita katika kufungua
milango ya biashara, kwa hiyo, hivi sasa wale wote wenye kiu ya
kujifunza na kufanya kazi ya uzalishaji tunawakaribisha hapa ili waweze
kufanya kazi hiyo ambayo itakuwa na manufaa sio kwao tu bali kwa taifa
pia,"aliongeza Ulega
Katika hatua nyingine, Waziri Ulega
amezitaka taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo ikiwemo Wakala ya Vyuo vya
Mafunzo ya Mifugo (LITA) na Wakala ya Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kubuni
mafunzo yatakayojumuisha watu wa elimu ya chini kabisa ambao wengi wao
ni darasa la Saba.
Alisema kwa sasa vijana ambao hawajasoma
wanakimbilia katika kuendesha Bodaboda kwa maana ndio njia wanayoiona
rahisi ya kujipatia kipato huku akizitaka taasisi hizo kuja na mkakati
maalum wa kuanzisha mafunzo ya kuwafundisha vijana hao fursa mbalimbali
zilizopo katika sekta hizo mbili na wakazitumia kujiajiri na kufanya
uzalishaji mkubwa utakaowezesha hata nchi kupata mapato.
Post A Comment: