Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk.Jabir Bakari akizungumza katika Banda National internet Data Centre alitembelea maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam kushoto kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa TCRA Lucy Mbogoro.
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA
ya Mawasiliano Tanzania imeweka bayana mpango wa kuwawezesha vijana
wabunifu katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kuibua bunifu nyingi
zaidi zitakazonufaisha uchumi wa nchi.
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
TCRA Dkt. Jabiri Bakari wakati akizungumza na waandishi wa Habari jijini
Dar es salaam.
Kuwe amesisitiza kuwa mwelekeo wa Uchumi unavutia
matumizi makubwa ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano na kusisitiza
kuwa vijana wenye ubunifu katika sekta ya Mawasiliano wanayo nafasi
kubwa ya kuchangia maendeleo ya uchumi wa Taifa.
“Tupo kwenye
zama za kidijitali; kwa hiyo mawazo na fikra kwa jinsi walivyo hawa
vijana ni tofauti na kipindi cha nyuma, vijana wanafikiri na kuona vitu
tofauti, kwa hiyo ni lazima tuweze kupata mambo mengi kutoka kwao
(vijana)” alisisitiza Kuwe.
Akizungumzia changamoto ya usalama
mtandaoni wakati huu Tanzania na dunia ikiwa katika mabadiliko makubwa
kwenye sekta ya Mawasiliano Mkurugenzi Mkuu huyo alisisitiza kuwa ni
wajibu wa kila Mwananchi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano
pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanakuja pamoja ili
kukomesha vitendo vya uhalifu mtandaoni.
Ili Tanzania iweze
kufikia azma ya kuwa na uchumi wa kidijitali usalama wa watumiaji huduma
za Mawasiliano kwenye mtandao ni suala ambalo Mamlaka ya Mawasiliano
inalitilia mkazo.
Alisisitiza kuwa Mamlaka kwa kushirikiana na
vyombo vingine vya ulinzi na usalama ipo macho wakati wote kuhakikisha
inadhibiti uhalifu mtandaoni kwa kuhakikisha wananchi wanapatiwa elimu
stahiki juu ya matumizi salama ya huduma za Mawasiliano mtandaoni.
“Mafanikio
ni mazuri kwa maana kwamba watu walikuwa wakipata meseji za kitapeli,
nataka nichukue muda huu kuwaeleza kwamba serikali iko kazini, Mamlaka
na sekta ziko kazini, tunavyozungumza hivi baadhi ya hao matapeli wengi
tu wapo kwenye vyombo vya sheria” alisema na kuongeza.
Kuwe
alisisitiza kuwa ni muhimu kwa upande wa wananchi wakashirikiana na
mamlaka pamoja na serikali kwa ujumla kwa kutoa taarifa za wahalifu wa
mtandaoni kwa kutuma ujumbe na namba za washukiwa wa utapeli kwenda
namba 15040 ili kutoa taarifa ya vitendo hivyo kwa shabaha ya kutokomeza
vitendo vya uhalifu kwenye mtandao.
Kuhusu zoezi la kuhakiki
namba za simu zilizosajiliwa na mtumiaji wa huduma za Mawasiliano ya
simu, Kuwe alisisitiza kuwa ni muhimu kila mtumiaji wa huduma za
Mawasiliano akahakikisha anahakiki namba zake zilizosajiliwa kwa
kutumia namba za kitambulisho cha Taifa kwa kubofya *106# kisha kufuata
maelekezo na hatimae kufuta usajili kwa namba ambazo mtumiaji atabaini
kutozitambua; ili kufuta namba za simu ambazo mtumiaji hazitambui
atapaswa kufika kwa wakala wa mtoa huduma za Mawasiliano ambae ndie
pekee aliepewa haki ya kufuta namba usizozitambua.
Akizungumzia
sababu za mtumiaji wa huduma za Mawasiliano kutopewa haki ya kuzifuta
namba za simu alizobaini kutozitambua kwenye simu yake; Mkuu wa Kitengo
cha Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano cha TCRA Thadayo Ringo alifafanua
kuwa hatua ya kutoruhusu mtumiaji kufuta namba asizozitambua inalenga
kumlinda mtumiaji kwa kuwa zoezi la kufuta namba hizo linahitaji
kuchukua alama ya kidole ili kuthibitisha kwamba anaetaka kufuta namba
ambazo hakuzitambua au ambazo asingependa kuendelea kuzimiliki.
Awali
Mkurugenzi Mkuu alibainisha kuwa TCRA inaweka mazingira wezeshi
kuhakikisha sekta ya Mawasiliano inakuwa na mchango mkubwa katika ukuaji
wa uchumi wa nchi.
Post A Comment: