NAIBU
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula
ameelekeza Shirika la Nyumba la Taifa NHC) kuipa kimpaumble mikoa ya
pembezoni kwa kujenga nyumba za makazi ili kuwawezesha wananchi pamoja
na watumishi wenye uhitaji.
Amewaelekeza kuwasiliana na viongozi
wa mikoa hiyo ambayo pia imepakana na nchi jirani ili waweze kujenga
nyumba hizo za makazi katika mikoa hiyo.
Mabula ametoa maelekeo
hayo leo Julai 27,2021 mkoani hapa wakati akizindua nyumba nafuu za
makazi zilizopo kata ya Mapupa Wilayani Masasi. Aliitaja baadhi ya mikoa
ya pembezoni kuwa ni Kigoma, Lindi, Mtwara na Ruvuma.
Mabula
amesema kuna uhitaji mkubwa sana wa nyumba za makazi kwa mikoa mingi
hasa ya pembezoni huku akimuelekeza Mwenyekiti wa Bodi kuhakikisha
wanaelekeza nguvu zaidi katika kujenga nyumba kwenye mikoa ya pembezoni.
“Kweli
nimeona kuna hitaji kubwa la nyumba za makazi na hasa kwa mkoa wa
mtwara, na mimi nielekele shirikka la nyumba, mwenye kiti wa bodi upo
hapa, , mikoa mingi iliyoko pembezoni ina shida sana ya nyumba za
makazi, na nyinyi ni shirika pekee ambalo tunalitegemea na kutarajia
kwamba litapunguza kero za nyumba,” amesema .
Ameongeza Serikali
inatarajia kuona kwamba shirika hilo kujenga walau nyumba sio chini ya
laki mbili kwa mwaka Hulu akifafanua shirika hilo halijaweza kufikia
idadi hiyo huku akisisitiza waongeza nguvu kwa kuwapa kipaumbele mikoa
ya pembezoni ili kuwawezesha wakazi wa maeneo ya mikoa hiyo wakiwemo
watumishi wa umma kupata nyumba za makazi.
“Watumishi wengi wana
hofu ya kwenda kufanya kazi katika mikoa hiyo kwa sababu hawana makazi
na hata wakipata makazi wankuwa mbali na eneo la kazi, kwa hiyo ni
vizuri mkawekeza katika maeneo hayo na mkaanza na mikoa ambayo
imeshaomba huduma hiyo ifanyike,” amesema.
Katika hatua nyingine, Mabula amepongeza na kushukuru shirika hilo kwa kazi kubwa wanayoifanya na za viwango nchini.
Akiwasilisha
taarifa ya ujenzi wa nyumba hizo, Mkurungezi Mkuu wa Shirika hilo Dk
Maulid Banyani amesema shirika hilo limejenga nyumba hamsini na nne
zenye thamani ya shilingi bilioni mbili. Amesema nyumba nyumba hizo ni
za kisasa kila moja ikiwa na vyumba vitatu.
Amesema nyumba hizo
ambazo zimejengwa kwa kutumia matofali maalumu zinapangishwa kila moja
kwa shilingi laki moja na nusu na kwamba zimekwisha kupangishwa zote.
Kwa
upande mwingine Dk.Banyani ameomba serikali iliwezeshe shirika hilo ili
waweze kuendelea kujenga nyumba nafuu za makazi kwa wananchi huku
akisema shirka hilo linaendelea kufanya jitihada zaidi kujenga nyumba
nafuu kwa mikao mbalimbali nchini.
Amesema kwa Mkoa wa Mtwara,
shirika hilo limeweza kujenga kutekeleza miradi ya nyumba yenye thamani
ya shiling bilioni kumi na tisa.
Home
Unlabelled
SHIRIKA LA NYUMBA LATAKIWA KUTOA KIPAMBELE KWA MIKOA YA PEMBEZONI KUJENGA NYUMBA ZA MAKAZI
Post A Comment: