Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Prof. James Mdoe akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji
wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu (STI) kwa ajili ya Maendeleo
Endelevu (SDGs) nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la
Uswidi (SIDA) na kutekelezwa kwa ushirikiano wa UNESCO, Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya
Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika
hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
Mkuu
wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO), Bi.Faith Shayo akizungumza kwa niaba ya
Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO nchini wakati wa uzinduzi wa mradi wa
uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu (STI) kwa ajili
ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya
Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika
hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
Mwakilishi
wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel akitoa
salamu za NATCOM wakati wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji wa mifumo ya
Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu
(SDGs) nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi
(SIDA) kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya Zanzibar pamoja na
Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Flomi
mjini Morogoro.
Mkuu
wa kitengo cha Sayansi Asilia wa UNESCO, Bw. Keven Robert akitoa
muhtasari wa mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na
ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania kwa
ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na
UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali ya Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM)
uliofanyika katika hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
James Mdoe (wa tatu kulia) akikata utepe kama ishara ya kuzindua mradi
wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa
ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania kwa ufadhili wa
Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
ya Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika
katika hoteli ya Flomi mjini Morogoro. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu
wa kitengo cha Sayansi Asilia wa UNESCO, Bw. Keven Robert (kushoto),
Mkuu wa kitengo cha Elimu wa UNESCO nchini, Bi.Faith Shayo (wa pili
kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel (kulia).
Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
James Mdoe (wa tatu kulia) akimkabidhi nakala ya mradi huo Afisa TEHAMA
wa TAMWA Bw. Godwin Assenga mara baada ya kuzinduliwa katika hafla
iliyofanyika hoteli ya Flomi mjini Morogoro. Wanaoshuhudia tukio hilo ni
Mkuu wa kitengo cha Sayansi Asilia wa UNESCO, Bw. Keven Robert
(kushoto), Mkuu wa kitengo cha Elimu wa UNESCO nchini, Bi.Faith Shayo
(wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya
Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel (kulia).
Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
James Mdoe (wa tatu kulia) akimkabidhi nakala ya mradi huo Afisa
Mtafiti kutoka idara ya DRCP (COSTECH) mara baada ya kuzinduliwa katika
hafla iliyofanyika hoteli ya Flomi mjini Morogoro. Wanaoshuhudia tukio
hilo ni Mkuu wa kitengo cha Sayansi Asilia wa UNESCO, Bw. Keven Robert
(kushoto), Mkuu wa kitengo cha Elimu wa UNESCO nchini, Bi.Faith Shayo
(wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya
Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(NATCOM-UNESCO) Bw. Joel Samwel (kulia).
Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma, Utafiti na Ubunifu wa (NM-AIST) Arusha,
Prof. Anthony Mshandete akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi wakati
wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi,
Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini
Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya Zanzibar pamoja na
Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Flomi
mjini Morogoro.
Baadhi
ya washiriki kutoka taasisi mbalimbali za sekta binafsi, serikali
pamoja na jamii walioshiriki uzinduzi wa mradi wa uimarishaji wa mifumo
ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu
(SDGs) nchini Tanzania unaoratibiwa na UNESCO kwa ufadhili wa Shirika
la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya
Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika
hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
Baadhi
ya vikundi kazi vilivyowashirikisha taasisi za elimu, watunga sheria,
watafiti, wizara, sekta binafsi, asasi za kiraia,jamii na vijana
wakijadili changamoto mbalimbali katika sekta ya Sayansi Teknolojia na
ubunifu wakati wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji wa mifumo ya Sayansi,
Teknolojia na ubunifu(STI) kwa ajili ya Maendeleo Endelevu (SDGs)
nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA)
kwa ushirikiano na UNESCO, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ya Zanzibar pamoja na Tume ya Taifa
ya Unesco (NATCOM) uliofanyika katika hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
Picha ya Pamoja
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe
amesema kuwa mpaka sasa hakuna sera ya sayansi , teknolojia na ubunifu
zaidi ya kuwa na sera ya sayansi ilitungwa mwaka 1996 ambayo ndio
inatumika kwa sasa.
Prof.
Mdoe aliyasema hayo jana mjini Morogoro wakati akizindua mradi wa
kuboresha mifumo ya sayansi, teknolojia na ubunifu kwa ufadhili wa
Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknololojia pamoja na Tume ya Taifa ya UNESCO.
Alisema
kuwa kama nchi na kwa kutambua umuhimu wa sayansi, teknolojia na
ubunifu kwa sasa mchakato wa kuandaa sera ya sayansi, teknolojia na
ubunifu unaendelea na kwamba wizara iko tayari kushirikiana na wadau
mbalimbali katika kukamilisha uandaaji wa sera hiyo.
“Covid
imetundisha tuwe tunajitegemea wenyewe kwa kuwekeza kwenye tafiti za
kisayansi na kama nchi mradi huu utasaidia tuko wapi na tunaelekea
wapi,” alisema Prof. Mdoe.
Awali
akitambulisha mradi huo Mkuu wa kitengo cha Sayansi asilia kutoka
UNESCO Keven Robert alisema kuwa mradi huo utawezesha kusaidia nchi
kuimarisha mifumo ya sayansi, teknolojia na utafiti.
Aidha
mradi huo pia utasaidia kuimarisha taasisi za kisayansi kufanya tafiti
na kuweka mazingira wezeshi ya kufanya tafiti za kisayansi ambazo
zitasaidia katika kutatua changamoto za wananchi, kukabiliana na majanga
yakiwemo magonjwa mbalimbali na pia kufikia malengo ya maendeleo
endelevu.
Robert
alisema kuwa mradi huo utakuwa na maeneo10 ya utekelezaji ambapo baadhi
ya maeneo ni pamoja na kuangalia uwekezaji katika tafiti za kisayansi
ambapo matokeo ya tafiti hizo zinapouzwa zinaweza kuimarisha uchumi ya
nchi.
“Mfano
katika kipindi hiki cha janga la Corona yapo mataifa yaliyofanya tafiti
za kisayansi na kutengeneza chanjo hivyo zinapouzwa mataifa hayo
yamekuwa yakipata fedha na kukua kiuchumi,” alisema Robert.
Alitaja
maeneo mengine yatakayoangaliwa katika mradi huo kuwa ni kwa namna gani
tafiti za kisanyansi zinasaidia wananchi na kwa namna gani wananchi
wanashirikishwa kwenye tafiti kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
Kwa
upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi mkazi wa UNESCO Faith Shayo
alisema kuwa mradi huo utakuwa wa awamu mbili na matarajio ya mradi huo
ni kuona nchi inazingatia maazimio 10 ambayo yaliazimiwa mwaka 2017
baada ya maazimo ya awali ya mwaka 1974 kufanyiwa maboresho.
Post A Comment: