Msajili Mwandamizi kutoka RITA, Rehema Mushi akitoa huduma kwa mwananchi waliofika katika banda hilo leo katika ya maonesho 45
ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya
Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari wa RITA, Edwin Mbekenga akitoa huduma kwa Wananchi waliojitokezaa kwenye banda la RITA katika maonesho 45
ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya
Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa wilaya ya Temeke mkoa wa Dar
es Salaam.
WAKALA
wa usajili ufilisi na udhamini RITA Ni moja ya Taasisi inayotoa na
inaendelea na huduma katika maonesho ya 45 ya Sabasaba. Hivyo
Wananchi wananufaika na maonyesho hayo huku wakijitoteza kwa wingi na
kuendelea kupata huduma ya vyeti vya kuzaliwa kwa urahisi zaidi mpaka
Sasa Wananchi waliojitokezaa na kufanya usajili huo takribani zaidi ya
wnanchi Elufu Moja na zaidi washajiandikisha na watapatiwa vyeti vyao
kabla ya maonyesho hayo kuisha, hivyo Wananchi mnakaribishwa kufika
kwenye viwanja hivi ili kupata fursa ya huduma za RITA kwa urahisi
na Ada yake ikiwa Ni shilingi 10000 tu, Amesema Msajili Mwandamizi
kutoka RITA, Rehema Mushi
Post A Comment: