Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akizungumza katika mkutano wa pamoja
baina ya Viongozi wa Mkoa huo na Wafanyabiashara wadogo wadogo.Mmoja
wa Wafanyabiashara wadogo wa Jiji la Dodoma aliyetambulika kwa jina la
Dangote akitoa maoni yake kwenye mkutano wa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Anthony Mtaka.
Wafanyabiashara
kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa
Mkoa, Anthony Mtaka katika mkutano wa pamoja uliolenga kutatua
changamoto za wafanyabiashara hao.
RC Mtaka ameyasema hayo jijini
Dodoma alipokua akizungumza na wafanyabiashara wadogo wadogo ambapo
ameahidi Serikali ya Mkoa itashughulikia changamoto ya taa za Barabarani
pamoja na kuhakikisha ulinzi wa uhakika unakuepo masaa yote.
Ametoa
kauli hiyo alipokua akijibu swali la mmoja wa wamachinga hao aliyeomba
kuongezewa kiwango cha muda wa kufanya Biashara zao, ndipo RC Mtaka
aliporuhusu kufanya biashara zao hadi asubuhi.
" Hili eneo la
Nyerere Square ambalo mnafanyia biashara hatuwezi kuwaongezea muda kama
mnavyotaka muwe mnaanza kufanya biashara asubuhi, hatufanyi hivyo kwa
kuwa hili ni eneo la Barabara ndio maana tukatoa kibali muwe mnaanza
biashara zenu hapa jioni.
Lakini sasa kwa kuwa Dodoma ni Jiji
tutaufanya mchana kuwa mrefu zaidi ya usiku kwa maana sasa mnaweza
kufanya biashara zenu hadi asubuhi, niwaahidi tutaboresha miundombinu ya
taa na patrol ya Polisi itakua inapita kuhakikisha usalama upo muda
wote," Amesema RC Mtaka.
Aidha RC Mtaka pia amewataka
wafanyabiashara hao wadogo wadogo kuzingatia sheria na kanuni za kufanya
kwao biashara ili wasilete athari kwa wananchi wengine wakati
wanatimiza majukumu yao.
RC Mtaka pia amewataka viongozi wa
Serikali kuanzia mamlaka za chini kutokuwa kikwazo kwa wafanyabiashara
hao na badala yake wawe sehemu ya kuwawezesha kukua kibiashara na
kufikia malengo yao.
Mkutano huo uliwahusisha Wafanyabiashara
wadogo kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma na kuhudhuriwa na
viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa Dk Fatma Mganga,
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma,Wakuu wa Wilaya na Mbunge wa
Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde.
Post A Comment: