Mkuu wa Mkoa wa Simiyu David kafulila amewataka wakuu wa wilaya katika mkoa huo kufungua milango ya ushirikiano na jamii ya wafanyabiashara ili kuchochea maendeleo katika Mkoa huo.
Amesema
kwa pamoja wanajukumu la kuchangamana katika kuleta maendeleo kwa
sababu jamii ya wafanyabiashara inamajibu mengi ya changamoto ambazo
zinaweza kukwamisha maendeleo.
Kafulila
ameyasema hayo alipokuwa katika hafla ya kumuaga aliyekuwa katibu
tawala wa Mkoa wa Simiyu Miriam Mbaga iliyofanyika Julai 5, na
kuhudhuliwa na wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Simiyu.
"ushirikiano huo utatumika kujenga mawazo mapya katika jamii,Isiwe
kwamba mkuu wa wilaya mtu aone kumfikia ni shida, hapana tengenezeni
milango ya kufikika ili mkutane mkae na kuzungumza maendeleo", alisema.
Aidha
amewataka wafanyabiashara kuendelea kushiriki katika kuinua ubora wa
elimu mkoani humo kwa kuichangia sekta ya elimu ili kuendelea kuwapa
nafasi zaidi wanafunzi waliopo katika madarasa ya mitihani kufanya
vizuri.
Katika hatua
nyingine kafulila amewataka wafanyabiashara wa zao la Pamba
kushirikikiana na wakulima wa zao hili katika kukifanya kilimo cha pamba
kuwa kilimo chenye tija ili kufikia malengo ya mkoa ya kuzalisha pamba
tani 500,000.
"Tuzidi kuchanga mawazo, tushirikiane, tumsaidie huyu mkulima tangu hatua za awali ilitija katika shughuli zao iongezeka".
Post A Comment: