MENEJA wa Benki ya NMB Tawi la Madaraka Jijini Tanga Elizaberth Chawinga akijiandaa kufunga kikapu  Mashindano ya Kikapu ya NMB Madaraka Cup yaliyoanza Jumamosi wiki hii kwenye viwanja vya Bandari Jijini Tanga ikiwa ni ishara ya ufunguzi wake
MENEJA wa Benki ya NMB Tawi la Madaraka Jijini Tanga Elizaberth Chawinga akifunga kikapu ikiwa ni ishara ya Ufunguzi wa Mashindano ya Kikapu ya NMB Madaraka Cup yaliyoanza Jumamosi wiki hii kwenye viwanja vya Bandari Jijini Tanga

MENEJA wa Benki ya NMB Tawi la Madaraka Jijini Tanga Elizaberth Chawinga kushoto akiwa ameshikilia mpira kabla ya kufunga 

MENEJA wa Benki ya NMB Tawi la Madaraka Jijini Tanga Elizaberth Chawinga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna walivyopania kuinua vipaji vya wana michezo mkoani Tanga
Mratibu wa Ligi hiyo Riziki Mgude alimaarufu “Kocha Bago” akieleza namna itakavyofanyika kwa siku za Jumamosi na Jumapili
MENEJA wa Benki ya NMB Tawi la Madaraka Jijini Tanga Elizaberth Chawinga kushoto akimkabidhi zawadi ya sh 30000 Kocha wa timu ya Jeshi la Uhamiaji Tanzania Asha Chenge ambaye alifunga mitupio huru mitatu kabla ya kuanza kwa mashindano hayo
Meza Kuu wakifuatilia matukio mbalimbali katika Mashindano hayo
Mchezaji wa Kikapu mkoani Tanga Patrick Semindu akizungumza kuhusu umuhimu wa mashindano hayo kwao

TIMU Harold wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Benki ya NMB kabla ya kuanza Ligi hiyo


TIMU Maximo wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Benki ya NMB kabla ya kuanza Ligi hiyo

 LIGI ya Mpira wa Kikapu ya NMB Madaraka Cup imeanza kutimua vumbi wikiendi hii kwenye viwanja vya Bandari Jijini Tanga huku Timu Harold wakiibuka na ushindi wa vikapu 78 -66 dhidi ya Maximo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mratibu wa Ligi hiyo Riziki Mgude alimaarufu “Kocha Bago”alisema lengo la kuanzisha mashindanbo hayo lilikujka kutokana na mazoezi waliokuwa wanayafanya kila Jumammosi saa kumi kwenye viwanja hivyo na walianza kuwa wengi wakaona watengeneze timu tatu ambazo zitakuwa na upinzani ili waweze kuanza kutengeneza ligi hiyo .

Alisema baada ya kufanikiwa kuanzisha ligi hiyo waliona wawafuate wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya NMB ambao walihaidi kuwadhamini Kombe na Medali lengo likiwa ni kukuza mchezo huo ili waweze kuendelea kufanya vizuri kwenye mashindano makubwa ikiwemo ya Taifa Cup.

Alisema kupitia ligi hiyo ambayo inachezwa kila wikiendi mpaka Septemba mwaka huu watakuwa wamepata wachezaji wazuri ambao wataweza kuwa tishio kwenye mashindano ya Taifa Cup na hivyo kufanya vizuri .

 “Lengo la kuanzisha Mashindano hayo kwanza ni kurudisha mchezo kwa wadau cha pili vijana waamini kwamba kupitia huko wanaweze kupata nafasi ya kuja kuwasaidia wengine ambao wapo chini yao”Alisema.

Awali akizungumza katika Mashindano hayo,Meneja wa NMB Tawi la Madaraka Jijini Tanga Elizaberth Chawinga alisema benki hiyo ipo kwenye nyanja tatu Elimu ,Michezo na Afya .

Alisema baada ya wao kufuatwa na Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Tanga ambao waliwaomba wawadhamini waliwakubalia na baadae na waliona waiitwe NMB Madaraka Cup.

“Sisi tupo kwa ajili ya kuendeleza vipaji michezo ni ajira na  afya na inatengeneza mahusiano na niwahaidi kwamba Benki ya NMB tutakuwa nanyi bega kwa bega na tunawakabribisha wengine wajitokeze”Alisema Meneja huyo.

Hata hivyo alitoa wito kwa wana michezo wengine iwapo wanahitaji kushirikiana nao milango ipo wazi na wamewasaidia vijana hawa kwa sababu wanajituma

“Tunaishukuru Serikali na wadau wa mkoa wa Tanga wanawaunga mkono hivyo kufungua milango kwa wengine wanaohitaji msaada ikiwemo mchezo wa pete”Alisema

Naye kwa upande wake Mchezaji wa timu ya mpira wa kikapu mkoani Tanga Patrick Semindu alisema uwepo wa mashindano hayo wao kama vijana unawaepusha na vitu mbalimbali ambavyo vingeweza kuwa hatarishi kwao.

Alisema michezo hiyo ina faida kubwa sana kwani kupitia michezo mtu anaweza kupata udhamini wa masomo ambao unaweza kuwa na tija kubwa sana kwake na kwa jamii inayomzunguka.

“Lakini pia mazoezi ni moja ya tiba na inaweza kuwasaidia wengi vijana wengi kupitia mchezo huo vijana wengi wanaweza kupata udhamini wa masomo na hivyo kupata manufaa makubwa”Alisema







Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: