NAIBU Waziri wa Maji (Mb) Mhandisi MaryPrisca Mahundi amesema kuwa kutokana na umuhimu wa michezo atahakikisha anashirikiana na  waandaji wa michuano ya mastara Cupnot2021 pamoja na kutafuta wadhamini wakubwa ili kukuza vipaji kwa vijana .

Mhandisi Mahundi amesema hayo jana wakati wa kuzindua michuano ya Mastara Cup 2021 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge Jijini Mbeya.

Willy Mastara ni mwandaaji wa michuano hiyo amesema mpaka sasa hajaweza kupata  wadhamini wa michuano hiyo.

Naye Mbunge wa Mbeya Mjini na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson amekubali kutoa zawadi zote za michuano hiyo baada ya kupokea ombi kutoka kwa mwandaaji hao.

Michuano hiyo mikubwa Jijini Mbeya inajumuisha timu thelethini na mbili hata hivyo waandaji hao walitoa  pongezi za kumbukuzi ya kuzaliwa kwake Mhandisi Maryprisca Mahundi.









 
Share To:

Post A Comment: