Naibu
Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (katikati) akiangalia madini
yaliyokatwa na kung'arishwa na kutengenezwa mapambo na urembo katika
Banda la Chuo cha Ufundi Stadi VETA mkoa wa Shinyanga kwenye Maonesho
ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya
Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkuu wa
Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa
Mara, Mhe. Ally Hapi.Kushoto
ni Mwalimu wa Chuo cha Ufundi Veta Shinyanga, Robert Onesmo akimwelezea
Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (katikati) kuhusu madini
yaliyokatwa na kung'arishwa na kutengenezwa mapambo na urembo katika
Chuo cha Ufundi Stadi VETA mkoa wa Shinyanga.
Madini yaliyokatwa na kung'arishwa na kutengenezwa mapambo na urembo katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA mkoa wa Shinyanga
Kaimu
Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele (kulia) akimwelezea Naibu
Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (wa pili kulia) kuhusu Mashine
zinazotumika kukata madini yenye uwezo wa kupitisha mwanga na yasiyo na
uwezo wa kupitisha mwanga.
Kaimu
Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele (kulia) akimwelezea Naibu
Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya kuhusu Fani ya Ufundi wa Mitambo
na magari makubwa
Mwalimu
wa Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga, Divoti Emmanuel akionesha vifaa
vinavyotumika katika ufundi wa mitambo mikubwa na magari makubwa kwenye
Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga,Veronica Mussa akielezea kuhusu Mfumo wa umeme majumbani kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
Mwanafunzi
wa Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga, Rose Silivery akielezea kuhusu
Mashine zinazotumika kukata madini yenye uwezo wa kupitisha mwanga na
yasiyo na uwezo wa kupitisha mwanga kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara
na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
Mwanafunzi
wa Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga, Amida Athumani akionesha madini
yaliyokatwa na kung'arishwa na kutengenezwa mapambo na urembo katika
Banda la Chuo cha Ufundi Stadi VETA mkoa wa Shinyanga kwenye Maonesho ya
Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Mwanafunzi
wa Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga, Husna Rashid akionesha vifaa
vinavyotumika katika urembo na upambaji kwenye Maonesho ya Pili ya
Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi VETA Shinyanga, Husna Rashid akionesha vifaa vinavyotumika katika urembo na upambaji kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
Naibu
Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya ametembelea Banda la Chuo cha
Ufundi Stadi VETA mkoa wa Shinyanga kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara
na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja
wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya
Shinyanga.
Naibu
Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya ametembelea banda hilo la Chuo
cha Veta wakati akifungua Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya
Madini Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Kassim Majaliwa Jumapili Julai 25,2021.
Akiwa
katika banda la Chuo cha VETA Shinyanga, Prof. Manya amejionea fani
mbalimbali zinazotolewa katika chuo ikiwemo Fani ya Uchongaji na
Ung'arishaji wa Madini ya Vito, Fani ya Umeme wa majumbani, Fani ya
Saluni na Mapambo na Fani ya Ufundi wa Mitambo na magari makubwa ambapo
ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuchangamkia fursa ya chuo hicho
kupata ujuzi mbalimbali.
Akielezea
kuhusu fani hizo, Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele
amesema chuo chao kinatoa mafunzo ya ukataji na ung'arishaji madini vito
pia mafunzo ya mitambo mizito katika uchimbaji wa madini akibainisha
kuwa VETA Shinyanga pekee ndiyo inatoa mafunzo ya aina hizo.
"Kwenye
banda letu tunaonyesha mafunzo yanayotolewa na VETA Shinyanga katika
fani za uchakataji madini (Ukataji na Ung'arishaji madini vito), Mitambo
mizito inayotumika katika uchimbaji madini (uendeshaji mitambo na
ufundi mitambo), fani ya umeme na fani ya Ulembeshaji (Salon) na mapambo
pia tunatoa huduma za Saluni na ukaguzi wa magari kwenye banda
letu",alieleza Mabelele.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Ally Hapi aliitaka VETA ianzishe
fani za madini kwenye mikoa mingine pia na kuipongeza VETA Shinyanga
kwa kuanza kutoa mafunzo katika sekta ya madini.
Maonesho
ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
yanayoongozwa na kauli mbiu “Uwekezaji wa Madini na Viwanda Shinyanga
kwa Uchumi Endelevu” yameanza tarehe 23 Julai, yanatarajiwa kuhitimishwa
tarehe 1 Agosti, 2021 katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa
kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Post A Comment: