Na Mwandishi wetu,Mbeya
NAIBU Waziri wa Maji na Mbunge wa Wanawake Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi ametembelea ujenzi wa jengo la machifu lililopo eneo la Nane Nane Jijini Mbeya.
Awali Chifu Roketi Mwanshinga alieleza maendeleo ya ujenzi akibainisha kusuasua kutokana na ukosefu wa fedha.
Katika kuwaunga mkono machifu Naibu Waziri Mhandisi Maryprisca Mahundi amejitolea malumalu za jengo lote ili jengo liwe na muonekana mzuri na wa kuvutia.
Post A Comment: