NAIBU
waziri wa maji ,Eng.MaryPrisca Mahundi amemuagiza katibu mkuu wa wizara
hiyo, atoe fedha za malipo kiasi cha sh .milioni 700 zilizoombwa na
Wakala wa usambazaji maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA)
wilaya ya Mkuranga ili kukamilisha ujenzi wa tanki la mradi wa maji
Mwanambaya.
Ameeleza mradi huu ni miongoni mwa miradi itakayonufaisha watu wengi kwani unakwenda kutoa huduma na kunufaisha watu 8,000 .
MaryPrisca
alitoa maagizo hayo wakati alipotembelea mradi wa chanzo cha maji
Mwanambaya na tanki,na kueleza fedha hiyo imeombwa mwezi Juni hivyo
wavute subira ,katibu mkuu afanyie kazi .
"Niisitize
miradi inayoelekezwa kutoa huduma kwa wananchi tunaendelea kuitolea
fedha kwa awamu hadi ikamilike ili kutimiza adhma ya serikali ya kumtua
ndoo mama kichwani na kuondosha kero sugu ya ukosefu wa upatikanaji wa
maji
Hata
hivyo ,ameielekeza RUWASA Mikoa na Wilaya kukamilisha miradi viporo kwa
wakati ili kurahisisha kazi ya usambazaji kwa wananchi .
Pia
MaryPrisca ,aliwaelekeza mameneja wa RUWASA mikoa na wilaya kuhakikisha
jumuiya za watumiaji maji vijijini wanapata watunza hazina makini
waliosoma uhasibu na kupata cheti ama diploma ili kutunza miradi
mbalimbali na iwe endelevu .
Nae
meneja wa RUWASA wilaya ya Mkuranga Maria Malale alisema ujenzi wa
mradi Mwanambaya umegharimu bilioni 2.3 ambapo bilioni 1.1 amelipwa
mkandarasi
Alisema mradi
umefikia asilimia 90 ,mkandarasi anaendelea na kazi licha ya kupelea
fedha milioni 700 ambayo wameshaiombea fedha kwa ajili ya malipo.
Mkuu
wa wilaya ya Mkuranga, Hadija Ally alisema ipo miradi inayoendelea
ambapo ikikamilika yote hali itakuwa safi na wananchi watanufaika kwa
kiasi kikubwa na upatikanaji wa maji mjini ni asilimia 86 na vijijini ni
76.
Katika ziara hiyo ya
kikazi ,MaryPrisca alitembelea na kukagua pia mradi wa maji Mkerezange
ambao umekamilika na upo kwenye matazamio .
Post A Comment: