Na Mwandishi wetu, Simanjiro
UONGOZI wa shule ya sekondari
Mgutwa umewasaidia wanafunzi wa chekecheka, wa darasa la kwanza na la
pili wa shule ya msingi Kandasikira Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,
waliokuwa wanakaa sakafuni kwa kukosa madawati, kwa kuwakabidhi viti na
meza hivyo kuondokana na kero hiyo.
Meneja wa shule ya sekondari
ya Mgutwa, Monica Mlemeta amesema wametoa msaada huo ikiwemo kalamu na
madaftari baada ya kubaini changamoto ya wanafunzi hao.Mlemeta amesema
walitoa msaada wa viti 25, meza 25, vitabu, kalamu na vifuto ili
kuwasaidia wanafunzi hao ambao wengi wao ni jamii ya watoto wa wafugaji
waohamahama kila mara.
Amesema wazazi wengi na walezi wa
wanafunzi hao wanaondoka na kuhama kufuata malisho ya mifugo yao hivyo
wanawaacha wanafunzi hao kwenye wakati mgumu.Meneja huyo amesema shule
ya sekondari Mgutwa ni majirani na shule hiyo ya msingi Kandasikira
hivyo walipokuwa wanawatembelea walikuta tatizo hilo kwa wanafunzi hao.
Amesema
wanamshukuru Mungu kwa hatua hiyo ila wanapaswa kuongeza msaada zaidi
ikiwemo chakula, kwani wanafunzi hao wanatakiwa kula shuleni hivyo
wasaidiwe. Amesema wanafunzi hao wanakabiliwa na changamoto ya kupata
uji wa saa nne na chakula cha mchana, ili waweze kusoka kwa bidii hivyo
wadau wa elimu wawasaidie hilo.
Amesema wanafunzi hao wanasoma
kwenye vyumba vya madarasa yasiyo na sakafu chini, hivyo wanakaa kwenye
madarasa yenye vumbi yanaymwagiwa maji ili wasome.
Post A Comment: