Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Wanawake
wa UWT Kibaha Mjini ,mkoani Pwani wanatarajia kuondokana na changamoto
ya ukosefu wa soko la uhakika mara baada ya kukamilika.kwa ujenzi wa
jengo la duka maalum la kuuzia bidhaa zao.
Ujenzi
wa duka hilo unatarajia kukamilika wakati wowote mwaka huu na
unatarajia kugharimu milioni 70 ,pamoja na hilo umoja huo umeanzisha
darasa la ujasiriamali ili kutoa elimu kwa akinamama.
Mwenyekiti
wa UWT Kibaha mjini, Elina Mgonja ,aliyaeleza hayo katika kongamano
lililoandaliwa na UWT Kibaha Mjini, kupongeza siku 100 na hotuba
aliyoitoa Rais Samia kwa wanawake pale Dodoma, Juni 8 mwaka huu.
Alisema
,tatizo kubwa kwa wanawake wajasiliamali ni soko hivyo wanaamini duka
hilo litawezesha kupeleka biashara zao na kuuzika huku wakijiinua
kiuchumi.
Aliomba wadau mbalimbali kujitokeza kuunga mkono ujenzi huo uweze kukamilika haraka.
Hata
hivyo ,Mgonja aliwaasa wanawake wamuunge mkono Rais Samia kwa kazi
kubwa ambayo ameanza kuionyesha ndani ya siku 100 kuwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Alisema,
maelekezo yaliyotolewa Dodoma kupitia mkutano wa wanawake wao wanafanya
kwa vitendo na kumhakikishia mwenyekiti wa CCM Taifa kuwa wataendelea
kumshika mkono mwanamke wa Kibaha ili kujiinua kimaendeleo.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Kibaha, Sara Msafiri ambae alimwakilisha
mkuu wa mkoa wa Pwani ,Aboubakar Kunenge ,Sara aliitaka UWT kuandaa
dawati la kusikiliza malalamiko ya akinamama kuhusu mirathi na ndoa ili
awasaidie upande wa wanasheria.
Pia alieleza vikundi vya ujasiriamali hufa kutokana na kukosa mshikamano ,amewapongeza wilaya hiyo kuwa na Umoja na mshikamano.
Nae
mbunge wa viti maalum mkoani Pwani ,Subira Mgalu alimpongeza Rais
Samia, kwa bajeti ya kwanza kupitishwa bungeni kwa asilimia kubwa,huku
akishukuru majimbo kupokea milioni 500 kila jimbo ambapo Pwani
imeshapokea bilioni 4.5 kwa majimbo Tisa.
Pia imetolewa bilioni 100 ili kukamilisha maboma ya vituo vya afya 1,500 nchini na zahanati hatua ambayo inahitaji pongezi.
Makamu
mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Selina Wilson alisema, kwa
kutambua vikundi vya ujasiriamali, halmashauri imetoa milioni 600 ndani
ya miezi sita ikiwa ni asilimia 60 kwa mikopo ya akina mama.
Post A Comment: