Makamu
waPili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwahakikishia
wadau wa maendeleo kutoka Swideni wanaoshughulikia miradi ya TASAF kuwa
serikali ya Mapinduzi Zanzibar itahakikisha miradi inayotekelezwa
inazingatia Thamani halisi ya Pesa inayotumika.
Mhe. Hemed akipata maelezo kutoka Bibi Annie Stomnge kutoka Swiden juu
ya azma yao ya kufanya ziara ya kukagua miradi mbali mbali ya TASAF
inayotekelezwa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali ya Mapinduzi
Zanzibar itaendelea kufanya vizuri katika utekelezaji wa miradi ya Mfuko
wa maendeleo ya Jamii (TASAF) ili kuwainua wananchi kiuchumi na
kujiongezea kipato.
Mhe. Hemed alieleza hayo wakati akizungumza
na wadau wa maendeleo wanaoshughulikia masuala ya TASAF kutoka Swiden
waliofika Afisini kwake Vuga Jijini Zanzibar.
Alisema serikali
inangalia uwezekano wa kuengeza nguvu katika sekta mbali mbali kwa ajili
ya kuwasaidia wananchi kupitia miradi ya TASAF.
Alibainisha
kwamba ujio wa ugeni huo utapata fursa ya kutosha ya kutembelea miradi
mbali mbali iliotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na viongozi
wanaosimamia TASAF Zanzibar.
Alisema kitendo cha ugeni huo
kwenda kujionea wenyewe katika maeneo yaliotekelezwa miradi hio
kutathibitisha jinsi gani Zanzibar ilivyojipanga kuinua hali za maisha
za wananchi wake.
Alisema miongoni mwa sekta watakazozitembelea
ni pamoja na sekta ya Afya na Elimu ili kuona kwa jinsi gani miradi
iliotekelezwa imesaidia jamii sambamba na kushauriana juu ya namba bora
ya kuweka vipau mbele kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mengine.
Akizungumzia
kuhusiana na Changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa miradi
hiyo Makamu wa Pili wa Rais alisema tayari Ofisi yake imeshatoa
maelekezo kwa watendaji wanaosimamia TASAF na baadhi ya changamoto
zimeanza kupatiwa ufumbuzi.
Mhe. Hemed alieleza kuwa serikali ya
awamu ya nane itahakikisha inasimamia kwa karibu katika kuhakikisha
thamani ya pesa inayotumika inaendana na miradi halisi inayotekelezwa.
Nae,
mdau wa maendeleo kutoka Swideni Bibi Annie Stomnge alimueleza Makamu
wa Pili wa Rais kuwa katika ziara yao hiyo watatembelea pia katika
maeneo yanayotumiwa kufanyika malipo kwa walengwa wa miradi sambamba na
kupata maoni kutoka kwa walengwa wa miradi hiyo.
Post A Comment: