Muonekano wa mashine zilizopo ndani ya kiwanda hicho.
Muonekano wa mashine zilizopo ndani ya kiwanda hicho.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali (Dkt) Gabriel Saul Mhidze (kulia)akimuelekeza jambo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel wakati wa ziara ya kutembelea kiwanda hicho.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel, akisalimiana na wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa MSD na wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Muonekano wa kiwanda hicho kwa nje.
Na Mwandishi Wetu, Njombe
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel ameipongeza MSD kwa jitihada inazozifanya za kuianzisha viwanda vya uzalishaji dawa na vifaa tiba nchini.
Dkt. Mollel ambaye ametembelea kiwanda cha MSD cha kuzalisha mipira ya mikono na vidonge huko Idofi, Makambako mkoani Njombe amesema hatua hiyo itaipunguzia serikali gharama za uagizaji wa bidhaa hizo kutoka nje ya nchi.
Ameongeza pia ujenzi wa viwanda hivyo ni njia ya kuelekea mafanikio ya pamoja ya kutatua changamoto za wananchi hususani katika upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali Gabriel Saul Mhidze (Dkt) amesema ujenzi wa viwanda utakamilika mwezi Septemba mwaka huu na uzalishaji unategemewa kuanza mwezi Oktoba mwaka huu.
Naye Msimamizi Mkuu wa mradi huo Bi. Selwa Ahmid amesema Kiwanda cha mipira ya mikono (Gloves) kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mipira 20,000 kwa saa, sawa na jozi 10,000.
Kwa upande wa kiwanda cha vidonge kitakuwa na uwezo wa kuzalisha vidonge 425,000 kwa saa na kiwanda cha dawa za Rangi mbili kitakuwa na uwezo wa kuzalisha vidonge 330,000 kwa saa huku dawa za maji (Syrup) zitazalishwa chupa 150 mpaka 180 kwa saa.
Post A Comment: