Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, akizungumza wakati akizindua Klabu ya NMB Mwanamke Jasiri jijini Mwanza.
Mkuu
wa Kitengo cha Biashara wa NMB, Alex Mgeni akipokea bidhaa
zilizosindikwa na Mjasiliamali, Doroth Kimati anayewezeshwa na NMB
katika uzinduzi wa Klabu ya ” NMB Mwanamke Jasiri” jijini Mwanza.
Katikati ni Mjasiliamali, Hellen Bugoye.
Baadhi ya akina mama wajasiriamali wakifuatilia hotuba mbalimbali kwenye uzinduzi wa Klabu ya NMB Mwanamke Jasiri jijini Mwanza.
Mkuu
wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza, Bi. Amina Makilagi amewaasa
wanawake wilayani humo kuchangamkia fursa zinazoletwa kwao na benki ya
NMB kwa maendeleo yao ya kiuchumi.
Mkuu
huyo wa wilaya aliyasema hayo alipokuwa anazungumza na umati wa
wanawake na wakazi wengine wa mkoa huo waliohudhuria uzinduzi wa klabu
ya ‘mwanamke jasiri’ mkoani Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla.
Bi.
Makilagi alisema kuwa wakazi wa Mwanza wasiache kuchangamikia fursa
zinazoletwa na benki ya NMB kwani benki hiyo ina malengo mazuri ya
kutaka kuleta maendeleo kwa wateja wake.
Aidha
Mkuu huyo wa wilaya aliwasihi sana wanawake kutoogopa kuchukua mikopo
ya NMB kwani ni mikopo rafiki sana na masharti yake sio magumu kabisa.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Biashara kutoka Benki ya NMB,
Alex Mgeni alisema lengo la kuzindua Klabu hii ni kuzidi kumpa ujasiri
mwanamke na wao kama benki kupata fursa ya kutoa mafunzo ya fedha kwa
wanawake ilikuwaongoza vyema katika ukuaji wao kiuchumi.
Bw.
Alex aliongeza kuwa ndani ya mwaka mmoja, benki hiyo imefanikiwa kutoa
mikopo ya bilioni 100 kwa wanawake zaidi ya 8000 Mkoani Mwanza huku
akiwakaribisha wateja wengine kufika ili kujipatia mikopo kwa manufaa
yao.
Post A Comment: