Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akiwa pamoja na
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Kipanga Juma Omary
pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Amos
Nungu wakimsikiliza mmoja wa wabunifu waliopo chini ya Tume ya Taifa ya
Sayansi na Teknolojia (COSTECH ) mara baada ya kutembelea banda la Tume
hiyo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akiongozana na
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH )
Dkt. Amos Nungu kutembelea banda la Tume hiyo katika Maonesho ya 45 ya
Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere
Dar es salaam.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akiwa pamoja na
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Kipanga Juma Omary
pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Amos
Nungu wakimsikiliza mmoja wa wabunifu waliopo chini ya Tume ya Taifa ya
Sayansi na Teknolojia (COSTECH ) mara baada ya kutembelea banda la Tume
hiyo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
TAASISI za Elimu nchini ikiwemo COSTECH zimekuwa na ubunifu unaolenga moja kwa moja kutatua changamoto katika jamii.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameyasema hayo
leo Julai 5,2021 alipotembelea banda la COSTECH katika maonesho ya 45
ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika katika viwanja vya
Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Amesema
COSTECH imekuwa ikiendeleza wabunifu kila mwaka kwani kumekuwa na
mashindano ya Maksatu na wale washindi wamekuwa wakiendelezwa.
"Nimefurahi
kuona kwamba zile nadharia ambazo zinafundishwa zinaenda mbali wanaweza
kufanya vitu kwa vitendo ambavyo moja kwa moja vinaenda kugusa katika
kujenga ujuzi unaomwezesha mtu kujiajiri au kuajiriwa katika sekta
ambazo zinagusa changamoto za Watanzania". Amesema Prof.Ndalichako.
Aidha
Prof.Ndalichako ametoa wito kwa wabunifu hasa wale ubunifu wao umefika
mbali kuwasiliana na COSTECH kupitia mitandao ya kijamii ama kufika
katika ofisi zao ili ubunifu wao utambuliwe na kuweza kusaidiwa kupitia
kambi za atamizi ambazo ziko COSTECH.
"Katika
ubunifu nyingi ambazo nimeziona zinalenga katika kutatua matatizo ya
kijamii kwahiyo nitoe wito kama kuna changamoto ya kimasoko pia nalo
tutashirikaiana na Wizara ya Viwanda na Biashara tuone ni namna gani
tunaweza kuwasaidia kuwatangaza zaidi ili waweze kupata wateja wengi na
biashara zao au ubunifu wao uweze kwenda kutoa mchango kwenye taifa
letu". Amesema Prof.Ndalichako.
Aidha COSTECH imekuwa mshindi wa pili katika maonesho ya mwaka huu.
Post A Comment: