Jane Edward, Arusha



Katika kuendelea kutunza vyanzo vya maji na matumizi endelevu ya rasilimali hizo katika kidakio Cha Kikuletwa ,mamlaka ya maji bonde la mto pangani kwa kushirikiana na wadau wa maji wamekutana jijini Arusha kuzungumza kwa pamoja juu ya ufanisi wa rasilimali hiyo ili iweze kuleta maendeleo katika uchumi.


Akizungumza na wanahabari mapema hii leo katika jukwaa la KWSP mwenyekiti wa taifa wa jukwaa la watumia maji nchini Tanzania, Injinia Mbogo Futakamba amesema ili kuweza kufika mbali Ni vyema wadau wakapanga pamoja ili rasilimali za maji ziwe endelevu.


Futakamba amebainisha  kuwa wadau wakikutana na kupanga pamoja itasaidia kuweka matumizi ya maji endelevu na kudhibiti matumizi mabaya ya maji,itasaidia sana kutunza upotevu wa maji. 



Nae Mkurugenzi wa bonde la mto pangani Injinia Segule Segule amesema kuwa jukwaa Hilo linahitaji ushirikishwaji wa watu ikiwa lengo Ni kujadili namna gani maji yanatumika kwa njia endelevu.


Ameongeza kuwa jukwaa hilo linahusisha watu wa sekta binafsi kwa lengo la kujadili namna gani ya kutunza maji ambayo yanapotea kila wakati, hususani katika viwanda. 


Abraham Yesaya Ni mratibu wa mradi huo amesema wizara ya maji kupitia bonde la mto pangani ipo kwenye mchakato wa kuhakikisha rasilimali za maji zinakuwa endelevu kwa njia ya ushirikishaji wa wadau,ikiwa Ni kupitia uundwaji wa majukwaa sambamba na mikakati ya kuelimisha wakulima ili waweze kutumia maji vizuri,kudhibiti uchafuzi,kutunza vyanzo vya maji na kudhibiti utupaji wa maji taka.


MWISHO...

Share To:

msumbanews

Post A Comment: