Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema wizara imefanikiwa kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu utambuzi wa wakulima ambapo hadi sasa kupitia Mfumo wa M-Kilimo tayari wakulima 1,979,662 na Maafisa Ugani 6,840 wamesajiliwa kwenye mfumo hatua inayosaidia kufikisha huduma za ugani na masoko kwa haraka.
Bashe
ametoa kauli hiyo jana(04.07.2021) wakati alipoongea na Waandishi wa
habari ofisini kwake Dodoma ambapo amesema lengo la wizara ya kilimo ni
kusajili wakulima takribani milioni 6 kupitia kaya zao hatua
itakayosaidia utambuzi na ufikwishwaji wa huduma za ugani ili kuwezesha
tija kwenye kilimo kupatikana.
Aliongeza
kusema kuwa ili wizara iweze kuwahudumia wakulima ni lazima kuwatambua
na kufahamu mahala walipo ndio maana ikaanzisha mfumo wa kiteknolojia wa
usajili wa wakulima (M-Kilimo) ambao sasa umefika mikoa yote ya
Tanzania Bara.
"
Katika bajeti ya mwaka 2021/22 wizara imepanga kufundisha maafisa ugani
(re-training) ili waweze kusaidia wakulima kuongeza tija kwenye
uzalishaji mazao ambapo ili lengo hilo lifanikiwe lazima uwatambue
wakulima ndio maana tumeanzisha mfumo huu wa Mobile Kilimo ambapo
wakulima wanasajiliwa kupitia maafisa ugani kwenye kata." aliema Bashe.
Akizunguza
juu ya umuhimu wa mfumo huo Naibu Waziri Bashe alisema mfumo M-Kilimo
utasaidia kupima kazi zaMaafisa ugani Kilimo katika maeneo ya kiutendaji
kwa kuwa takwimu zinaonesha kila ushauri alioutoa kwa mkulima ikiwa ni
wa ana kwa ana (physical consultation) au kupitia njia ya mtandao
(online consultation).
“
Hadi sasa jumla ya maswali ya wakulima yapatayo 7,792 yamepokelewa na
kujibiwa na maafisa Ugani Kilimo kupitia mfumo wa M-Kilimo unaoratibiwa
na Wizara ya Kilimo” alisisitiza Bashe na kuongeza kuwa wizara
inatarajia kufungua kituo cha huduma kwa wakulima (Call Centre)
kuwezesha wakulima kupiga simu na kujibiwa maswali yao kwa haraka zaidi.
Katika
hatua nyingine Bashe ametaja mikoa iliyofanya vizuri kwenye usajili wa
wakulima kuwa ni Morogoro (153,977), Njombe (153,158) na Mara (148,772)
huku mikoa ambayo bado ipo chini ikiwa ni Pwani imesajili wakulima
14,784) na Mtwara (28,000) .
Kufuatia
hatua hiyo Bashe ametoa wito kwa wakurugenzi wa halmashauri nchini
kuwawezesha maafisa ugani wao wa wilaya kusajili na kuhamasisha wakulima
ili waingie kwenye mfumo wa M-Kilimo kuwezesha kufikia lengo la kukuza
tija kwenye uzalishaji mazao ya kilimo kupitia huduma bora za ugani.
Ili
kuleta ufanisi kwenye usajili wa wakulima Naibu Waziri huyo wa wizara
ya Kilimo alisema kupitia bajeti 2021/22 inatarajia kununua simu za
mkononi za kisasa (smartphones ) na kuzigawa kwa Maafisa Ugani kote
nchini ili zitumike kusajili wakulima kwa kutumia teknolojia maalum
(App)
Naye
Mratibu wa Mfumo wa M-Kilimo Rajab Mkalange amesema mfumo huu ni wa
kiteknolojia unaoweza kumsaidia mkulima kupata huduma za ugani na masoko
kupitia maswali kwenye simu yake ya kiganjani kuwasiliana na Afisa
Ugani ngazi za kijiji, kata, wilaya na Wizarani.
Aliongeza
kusema mfumo huu tangu uliopanza kufanya kazi mwanzoni mwa mwaka huu
umewezesha kupunguza tatizo la upungufu wa maafisa ugani kwa kuwa
wakulima wanaweza kupata huduma hizo pale wanapokuwa wamesajiliwa kwenye
mfumo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mifumo ESRF John Kajiba alisema taasisi yake
ilifanya utafiti kwenye mikoa ya Kagera na Mara kuhusu mahitaji ya
wakulima kwenye huduma za ugani na kugundua kuwa wakulima wanahitaji
taarifa za huduma za ugani na masoko kwa haraka kutaboresha tija kwenye
Kilimo.
Kajiba
aliongeza kusema kuwa kupitia utafiti huo ndipo wakaanzisha ushirikiano
na Wizara ya Kilimo kuanzisha mfumo wa M-Kilimo unaotekelezwa kote
nchini .
Wakulima
wanaweza kujiunga na Mfumo wa M-Kilimo kupitia simu zao za mkononi
ambapo wanaweza kubonyeza *152*00# na kuchagua neon Huduma za Serikali
kisha kubofya namba 7 Kilimo.
Mwisho
Imeandaliwa na :
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo
Post A Comment: