Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha
Serikali
kupitia Wizara ya Kilimo imepitisha mbinu ya kukuza uwekezaji unaolengwa
kuelekea mnyororo wa maalum wa thamani hususani katika kuboresha uzalishaji.
Waziri
wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo tarehe 11 Juni 2021 wakati
akizungumza kwenye Mkutano wa wawekezaji wa Ulaya katika jukwaa la kilimo.
Amesema
kuwa uzalishaji mdogo wa mazao umekuwa tatizo kubwa kwa wakulima nchini, ingawa
tayari serikali imeboresha upatikanaji wa pembejeo ikiwemo mbegu, mbolea pamoja
na viuatilifu.
Waziri
Mkenda amesema kuwa serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo
Awamu ya II (ASDP II) kwa kipindi cha mwaka 2017-2020 imeondoa/kufuta ada
takribani 105, na tozo ambazo zilitozwa na bodi mbalimbali za mazao na taasisi
za kilimo.
“Pia
tumechukua hatua kadhaa kurekebisha Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, 1982
kupitia Sheria ya Fedha, 2017 ambayo inapunguza mazao kuanzia asilimia 5 hadi 3
ili kupunguza gharama za kufanya biashara kwa wawekezaji katika sekta ya
kilimo” Amekaririwa Prof Mkenda
Pia
Waziri Mkenda amesema kuwa ili kuimarisha sekta ya kilimo nchini serikali imepunguza
ada ya upimaji wa mbolea wakati wa usajili. Ada ya upimaji ilikuwa ya juu kama
USD ya 300,000 na waombaji walihitaji msimu wa tatu (3) kuthibitisha ufanisi
wake ambapo ada hiyo ya upimaji imepunguzwa hadi kufikia 100,000
Prof
Mkenda amesema kuwa lengo la kupunguza ada hiyo ni kufanya kilimo kuwa na ustahimilivu,
jumuishi, yenye ufanisi na mwitikio wa soko kote nchini.
Amesema
kuwa chini ya ASDP II, Wizara ya Kilimo inashirikisha wadau wote ikiwa ni
pamoja na sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wa maendeleo
katika maeneo mbalimbali kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa hadi taifa hadi ili
kuwezesha mbinu itakayopelekea kuwa na maendeleo endelevu ya kilimo.
Amesema
kuwa ASDP II inakuwa sehemu ya mnyororo wa maendeleo ya sekta ya kilimo kwa
kuunganisha malengo ya CAADP na kuakisi zaidi maono na kanuni zinazoendana na
maelekezo ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi, FYDP na hotuba yenye maono ya
Tanzania endelevu iliyotolewa Bungeni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya mboga na matunda-TAHA Dkt Jacqueline Mkindi
amesema kuwa mkutano huo umekuwa ni fursa kubwa ya kuwaweka karibu na serikali wawekezaji
wa sekta ya mboga na matunda kwani watatumika kama chachu ya kuwaalika
wawekezaji wengine kuja nchini.
Amesema
kuwa wawekezaji wote nchini wana furaha kubwa kutokana na serikali kuyaeleza
kwa ufanisi ikiwemo kuondoa mambo karibu nane kwenye bajeti yam waka 2021/2022 yahusuyo
ushuru pamoja tozo ambazo hazikuwa rafiki katika sekta hiyo.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa jukwaa la kilimo la wawekezaji wa bara la Ulaya Bi Cikay Richard
ameeleza kuwa mkutano huo umewakutanisha wawekezaji wa Kilimo kutoka bara la Ulaya
ambao kwa kiasi kikubwa wameeleza changamoto ambazo zinawakabili hususani
katika sekta ya mboga na matunda (Horticulture).
Ameongeza
kuwa mjadala mkubwa zaidi katika mkutano huo umejikita katika kutafakari kwa
pamoja namna ya kuimarisha sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa na faida ya jumla
kwa wawekezaji lakini kuimarisha pato la kigeni kwa serikali.
Kadhalika,
Mkurugenzi wa kampuni ya Hortanzia Afrika Sun Fruit Bw Rory Nightingale na Mkurugenzi
wa Kampuni ya YYTZ Bw Fahad Awadh wameipongeza serikali kwa dhamira yake ya
dhati kukutana na wawekezaji ili kusikiliza na kutatua changamoto
zinazowakabili.
MWISHO
Post A Comment: