Mkuu wa Shughuli za Uwekaji Vinasaba (TBS),Mhandisi Florian Batakanwa akizungumza mara baada ya kukabidhi mashine za kutambua kiasi cha kinasaba kwenye mafuta hasahasa kwenye soko la ndani ikiwemo Petrol Station kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo Jijini Dar es Salaam.

Meneja Ufundi idara ya Petrol (EWURA), Mhandisi Shaban Selemani akizungumza mara baada ya kupokea mashine za kutambua kiasi cha kinasaba kwenye mafuta hasahasa kwenye soko la ndani ikiwemo Petrol Station kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) leo Jijini Dar es Salaam.

Moja ya maabara zinayotembea zenye mashine za kutambua kiasi cha kinasaba kwenye mafuta hasahasa kwenye soko la ndani ikiwemo Petrol Station ambazo Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limekabidhi kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) .

**************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limekabidhi mashine za kutambua kiasi cha kinasaba kwenye mafuta hasahasa kwenye soko la ndani ikiwemo Petrol Station kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) .

Wamekabidhi maabara zinazotembea mbili pia na mashine mbili zingine ambazo zitakuwa zinaangalia kama itatokea katika kufanyakazi kuna mashine ambayo imeharibika watafanya mabadiliko ili zoezi liweze kuendelea.

Ameyasema hayo leo Mkuu wa Shughuli za Uwekaji Vinasaba (TBS),Mhandisi Florian Batakanwa akikabidhi mashine hizo leo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Mhandisi Batakanwa amesema baada ya zoezi hilo kufanyika tayari kwenye masoko pamoja na kwenye petrol station zote nchini wana magari kwaajili ya kwenda kufanya utambuzi wa kinasaba.

"Hii itaweza kutusaidia kutambua mafuta ambayo hayajakidhi ubora au yamechanganywa na mafuta mengine. Maabara hizi zinatembea na ndani ya gari kuna mashine kwaajili ya kufanya utambuzi, kuna kompyuta ya kuendesha mashine pamoja na vifaa vya kuweza kutuonesha maeneo hayo au GPS". Amesema Mhandisi Batakanwa.

Kwa upande wake Meneja Ufundi idara ya Petrol (EWURA), Mhandisi Shaban Selemani amesema wataendelea kuhakikisha mafuta yote yanayosambazwa hapa nchini kukidhi viwango vya ubora ili kutoharibu magari na mitambo mingine inayotumia mafuta na vilevile biashara kufanyika kwa uhalali.

"Vifaa hivi ni sehemu ya kutusaidia tuweze kuendelea kulisimamia zoezi hili ili kuhakikisha mafuta yanayosambazwa nchini yamekidhi viwango vya ubora unaotakiwa". Amesema Mhandisi Selemani.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: