Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akijaribu mashine maalumu ya kuoteshea alizeti, wakati alipokuwa akitembelea mabanda katika mkutano na wadau wa zao la alizeti, uliofanyika  mkoani hapa leo. Kulia ni Meneja wa Wakulima  Wadogo kutoka Kampuni ya Pyxus, Edwin Shio 

Waziri wa Kilimo Profesa, Adolf Mkenda, akizungumza kwenye mkutano huo. 

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Andrew Masawe, akizungumza kwenye mkutano huo. 

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Binilith Mahenge, akizungumza kwenye mkutano huo. 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba, akizungumza kwenye mkutano huo. 

Mbunge wa Singida Mjini, Musa Sima, akizungumza kwenye mkutano huo. 
Wabunge wakiwa kwenye mkutano huo.
Wabunge wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia, mbegu katika banda la Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA).

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, akimuelekeza jambo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea banda la Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia mafuta yanayotokana na zao la alizeti yanayotengenezwa na Kampuni ya Singida Fresh Oil Mill, wakati alipotembelea mabanda, kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.

Wadau wa kilimo wakiwa kwenye mkutano huo. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa  Asasi kilele ya sekta binafsi inayojihusisha na kuendeleza tasnia ya horticulture hapa nchini ijulikanayo kama TAHA, Dkt. Jacqueline Mkindi, na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Sekta Binafsi,  Francis Nanai.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo alipotembelea banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani hapa.


 Na Dotto Mwaibale, Singida


SERIKALI hutumia Sh. Bilioni 474.  hapa nchini kwa ajili ya kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi. 

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  wakati akifungua mkutano wa wadau wa Tasnia ya Alizeti kutoka Mkoa wa Singida, Simiyu na Dodoma uliofanyika mkoani Singida leo.

"Hapa nchini kuna mazao na bidhaa ambazo hatujitoshelezi hivyo kulazimika kuagiza kutoka nje ya nchi bidhaa hizo ni pamoja na mafuta ya kula ambayo mahitaji yake yanakadiriwa kuwa ni tani 650,00 na uzalishaji wa ndani ni wastani wa tani 290,000 sawa na asilimia 45 ya mahitaji kwa mwaka hivyo, nchi hulazimika kuagiza wastani wa tani 360,000 hadi tani 400,000 kwa mwaka kufidia upungufu huo ambapo hugharimu takribani Shilingi bilioni 474," alisema Majaliwa. 

Majaliwa alisema kutokana na umuhimu wa mafuta ya kula, Serikali imeweka mkakati wa kuongeza uzalishaji wa mazao ya mafuta yakiwemo chikichiki, alizeti, pamba, karanga na ufuta ili kujitosheleza na kuondokana na uagizaji wa mafuta kutoka nje ya nchi.

 Alisema hatua za awali zilizofanyika ni kutekeleza mikakati ya kuendeleza zao la michikichi kwa kuweka nguvu katika Mkoa wa Kigoma ambapo kilianzishwa Kituo Maalum cha Utafiti wa Mchikichi cha Kihinga na kupitia utafiti huo yameanza kuona matokeo makubwa ya uzalishaji wa miche bora yenye uwezo wa kuzalisha mafuta kiasi cha wastani wa tani 5 kwa hekta ikilinganishwa na aina ya michikichi ya zamani iliyopo sasa inayozalisha wastani wa mafuta ya mawese tani 1.6 kwa hekta. 

Majaliwa alisema kuwa hadi kufikia Mei, 2021 jumla ya mbegu 5,630,376 za chikichi na miche milioni 1.5 imezalishwa na kusambazwa katika Mikoa ya Kigoma, Katavi, Kagera, Rukwa, Mbeya, Pwani na Ruvuma. 

Waziri Mkuu Majaliwa alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa Serikali imeendelea kutoa kipaumbele cha kuendeleza sekta ya kilimo kuanzia ngazi ya uzalishaji, viwanda na masoko na hiyo inatokana na ukweli kwamba takribani asilimia 70 ya watanzania wanajishughulisha na kilimo na kuwa katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wameendelea kufanyia kazi changamoto zilizopo kwenye mazao ya kilimo hatua kwa hatua kwa kuwasikiliza wadau, kupata maoni yao na kukubaliana mikakati thabiti ya kuendeleza mazao katika mnyororo wa thamani. 

 Aidha Majaliwa alisema kuwa serikali mbali ya kufanya utafiti inatoa huduma za ugani, upatikanaji wa mbegu bora na viuatilifu, kuongeza matumizi ya zana zana bora za kilimo, kuwajengea uwezo wazalishaji kuhusu kanuni za kilimo bora, kuanzisha mfumo imara wa ugharamiaji wa mazao ya mafuta kwa kushirikisha taasisi za fedha. 

Alisema kufuatia hatua hiyo ni matarajio ya Serikali kuwa mikakati hiyo itawezesha kuongeza uzalishaji kutoka wastani wa tani 649,437 hadi tani 1,500,000 za alizeti zitakazochangia upatikanaji wa mafuta kwa takribani tani 300,000 ifikapo mwaka 2025. 

Alitaja mikakati mingine ya Serikali kuwa ni kuendelea kuwekeza katika Taasisi zinazohusika na utafiti na uzalishaji wa mbegu ili kuongeza tija na kuwa kwa kuzingatia umuhimu mbegu, Serikali imeongeza bajeti ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kutoka Shilingi bilioni 7.35 mwaka 2020/2021 hadi Shilingi bilioni 11.63 mwaka 2021/2022. Vilevile, bajeti ya Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) imeongezeka kutoka bilioni 5.42 mwaka 2020/2021 hadi Shilingi bilioni 10.58 mwaka 2021/2022 ili kuongeza upatikanaji wa mbegu bora zikiwemo mbegu za mazao ya mafuta ya kula. 


Share To:

Post A Comment: