MKUU wa Mkoa wa Tanga Adamu Malima akizungumza wakati akizundua wiki ya unywaji maziwa iliyofanyika
kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga |
Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania
Dkt. George Msalya akizungumza wakati wa uzinduzi huo |
Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania
Dkt. George Msalya akifuatilia jambo kwa umakini wakati wa maonyesho hayo |
KAIMU Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko Steven Michael ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu (M) Prof.Elisante ole Gabriel akifuatia jambo wakati wa uzinduzi huo |
MKUU wa Mkoa wa Tanga Adamu Malima katika akiwa Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko Steven Michael ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu (M) Prof.Elisante ole Gabriel kulia na kushoto ni Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Dkt. George Msalya wakigawa maziwa kwa wanafunzi wa shule mbalimbali Jijini Tanga wakati wa uzinduzi wa wiki ya wiki ya unywaji maziwa iliyofanyika kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga
Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Dkt. George Msalya akigawa maziwa wakati wa uzinduzi wa wiki ya umywaji maziwa kwenye viwanja vya Tangamano Jijini Tanga kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko Steven Michael ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu (M) Prof.Elisante ole GabrielMsajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Dkt. George Msalya katika akiwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shillow akigawa maziwa
Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Dkt. George Msalya kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima wakinywa maziwa wakati wa uzinduzi huo
Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko Steven Michael ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu (M) Prof.Elisante ole Gabriel akinywa maziwa wakati wa uzinduzi huo |
Wanafunzi wa shule mbalimbali za Sekondari na Msingi Jijini Tanga wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwenye viwanja vya Tangamano kwa ajili ya uzinduzi wa wiki ya Maziwa iliyofanyika kwenye viwanja hivyo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima amewataka wafugaji
kujiunga kwenye vyama vya ushirika vya ufugaji ili serikali na taasisi
mbalimbali ziweze kuwafikia kirahisi kwa kuwapatia huduma zikiwemo za
kifedha ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Malima
aliyasema hayo wakati akizundua wiki ya unywaji maziwa iliyofanyika
kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga ambapo alisema wakihimizana
kupitia vyama vya ushirikia wanaweza kuwa na mikakati ya makusudi kwa
ajili ya kuendeleza sekta hiyo.
Alisema
sekta hiyo ina mchango mkubwa sana hivyo upo umuhimu wa wafugaji hao
kuona namna nzuri ya kuweza kujiunga kupitia vyama vya ushirika ili
waweze kupata mafanikio mbalimbali ikiwemo ya kuweza kupata fursa za
mikopo kupitia taasisi za kifedha zilizopo nchini.
“Ndugu
zangu wafugaji lazima tubadilike na kuona umuhimu wa kujiunga na vyama
vya ushirika badala ya kuwa pekee yenu kwani kujiunga huko kutawasaidia
na kuwa rahisi kwa serikali kuwafikia sambamba na taasisi mbalimbali za
kifedha kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi” Alisema
Hata
hivyo aliwataka wazalishaji hao waongeze uzalishaji wa maziwa kutokana
na kwamba wadau wakubwa ni watoto na lazima wawe na idadi kubwa ya
watumiaji huku akitoa wito kwa wazazi na walezi kutambua kwamba suala la
maziwa ni muhimu kwa watoto kama anavyokula chakula.
Mkuu
huyo wa Mkoa aliwataka wafugaji na wazalishaji wa maziwa wawe na
uratatibu wa kupunguza bei ya maziwa na kuongeza uzalishaji wenye tija
ili bei ya maziwa ishuke.
Hata
hivyo alimuagiza Afisa uzalishaji Mkoa wa Tanga kukutana na wazalishaji
wa mkoa na hao wazalishaji wakafanye hesabu juu ya namna Tanga
inawezeje kuwa mzalishaji mkubwa wa maziwa kwa kuwa kuna mwamko mkubwa
wa uzalishaji wa ng'ombe kutokana na kwamba sekta ya maziwa bado ina
nafasi kubwa sana.
Awali
akizungumza wakati wa uzinduzi huo Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania
Dkt. George Msalya alisema lengo la bodi ya maziwa ni kusimamia na
kuratibu tasnia ya maziwa nchini kutokana na kwamba ni muhimu kwa
maendeleo haya kiuchumi kwa sababu ni biashara na lishe.
Alisema
bodi hiyo inaratibu shughuli zote ambapo alisema kuhusu wiki ya unywaji
maziwa dunia kote inapofika June 1 nchi nyingi zinahamasisha watu
kunywa maziwa hivyo wanaungana na hapa nchini watu wanakunywa maziwa
kidogo sana
Alisema
takwimu za Tanzania mwaka jana kwa mtanzania mmoja anakunywa maziwa lita
54 kwa mwaka lakini shirika la afya la umoja wa mataifa wanapendekeza
kwamba ili angalau uweze kupata virutubisho vya kutosha ni angalau
ukanywa maziwa lita 200 kwa mwaka
Aliongeza
kwamba uzalishaji wa maziwa kwa sasa ni lita bilioni 3.4 takwimu za
mwaka jana ukichukua kiasi hicho cha maziwa na idadi ya watanzania
milioni 60 utagundua watanzania wanakunywa maziwa kidogo
Hata
hivyo kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Wafugaji wa
Ng'ombe wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU) Shamte Saidi alisema unywaji wa
maziwa upo chini lakini uzalishaji bado hawajafikia kiwango ambacho
kitaweza kuhakikisha watanzania wanaweza kupata lita mbili kwa wananchi
na ndio maana kauli mbiu ikasema tuongoze uzalishaji.
Mwisho.
Post A Comment: