Na Mwandishi wetu , Dodoma
RAIS wa Jamuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluu Hassan be amempongeza, Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa kuhakikisha anashughulikia kero za maji huku akijitahidi kujibu maswali ya wabunge kwa weledi hoja zinazohusu sekta hiyo bungeni.
Rais Samia ametoa kauli jana wakati akizungumza na Wanawake wa Tanzania jijini Dodoma,ambapo amesema Mhandisi Mahundi amekuwa mchapakazi ambaye anapobaini kero au tatizo la maji katika eneo husika yeye kwa kushirikiana na Waziri wake, Juma Aweso huyafikia maeneo hayo na kushughulikia mara moja.
“Kama mnavyosikia na kuona katika bunge kilio kikubwa ni maji maswali mengi yameelekezwa huko Mary Mahundi, Naibu wangu anajibu mpaka uwa namuangalia nacheka na kimo chake na maswali anayoyajibu bungeni lakini akitoka hapo ni mbio kwenye maeneo ya maji , yeye upande wake na Wziri wake upande wake,” amesema Rais Samia.
Amesema tangu uhuru hadi uongozi wa awamu ya tano , waliweza kupeleka maji kwa watanzania asimilia 74 na kwamba hadi sasa wanakabiliwa uhaba wa maji kwa asimilia 26 lakini wanaendelea kuendelea kupeleka maji katika maeneo mbalimbali nchini kama ambavyo Waziri wa Maji anavyosema kwenye vikao vya Bunge.
Aidha Rais Samia amewahakikishia watanzania kuwa itakapofika mwaka 2025 Serikali itakuwa imekamilisha yale yote yaliyo kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi kupeleka maji katika miji na majiji kwa asilimia 95 na vijijini asilimia 85 lengo likiwa ni kumtua mama ndoo kichwani.
Mwisho.
Post A Comment: