Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila amewasisitiza viongozi wapya wa Serikali ya Wanafunzi -MASO kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali iliyopo.
Prof. Mwakalila ametoa kauli hiyo jjijini Dar es Salaam kampasi ya Kivukoni wakati akimwapisha Rais na Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi na kusema kuwa uongozi ni uadilifu, ushirikishwaji hivyo viongozi hao lazima wajue dhamana waliyonayo.
Pia Prof. Mwakalila amewasihi viongozi hao kujiepusha na migogoro,makundi yasiyo na tija na badala wazingatie zaidi kile ambacho kimefanya wawepo chuoni hapo.
"Kazi kuu iliyowaleta hapa Chuoni ni kusoma, hivyo pamoja na mambo mengine hakikisheni mnakuwa mfano kwa wengine na ikiwezekana fanyeni vizuri zaidi katika masomo yenu na mpate daraja la kwanza," alisisitiza Prof. Mwakalila.
Viongozi waliapishwa leo na Mkuu wa Chuo ni Rais wa wanafunzi Godson Peter na Makamu wa Rais Jekung'una Hafsat, ambapo uongozi wa Chuo umewatakia kila lakheri katika kutimiza majukumu yao.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mahusiano-
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
16.06.2021
Post A Comment: