Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick  Ndahani, ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza wakati akifunga mafunzo ya waelimishaji rika wa Mradi wa TIMIZA MALENGO unaotekelezwa na Amref Tanzania mkoani hapa jana.
Waelimishaji rika wa Mradi wa TIMIZA MALENGO unaotekelezwa na Amref Tanzania mkoani hapa wakimsikiliza, Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick  Ndahani, wakati akifunga mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yakifungwa.
Mafunzo yakifungwa.



Na Dotto Mwaibale, Singida


KAIMU Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick  Ndahani awewaomba vijana Wasichana ambao ni waelimisha rika kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi kwa vijana wa mkoa wa singida.

Ombi hilo limetolewa na Ndahani ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati akifunga mafunzo ya waelimishaji rika wa Mradi wa TIMIZA MALENGO unaotekelezwa na Amref Tanzania ambapo jumla ya waelimishaji rika 51  wasichana waliozalia nyumbani  kutoka Halmashauri ya Iramba, Singidana Manispaaa wamepatiwa mafunzo ya malezi bora ya watoto na familia.

Ndahani alisema kuzaa nyumbani siyo mwisho wa mafanikio katika maisha ,vijana wanapaswa kutumia changamoto walizonazo na kuzibadili kuwa fursa kwani wasichana wengi wakishazaa hukataka tamaa na mwisho kushindwa kuhudumia watoto wao na familia kwa ujumla.

Kaimu Afisa Maendeleo huyo amewashauri wasichana kuunda vikundi vya ujasiriamali katika maeneo yao ili kujipatia kipato kwani mkoa wa singida unazo fursa nyingi za kiuchumi kama vile ufugaji wa kuku wa asili, nyuki na kilimo cha mboga na mazao mengine kama Alizeti, mahindi, mpunga na dengu.

" Hatupendi kuona wala kusikia msichana au mwanamke anakuwa maskini  katika nchi hii ili  hali Rais wa Tanzania ni   Mwanamke lazima wanawake hapa nchini wawe wa mfano katika Bara la Afrika kwa sababu tunaye Rais mwanamke ambaye ni mchapakazi na makini katika uogozi ambaye anawajali wanawake na katika kuonesha hilo mapema wiki hii alikutana nao mkoani Dodoma na kuzungumza nao," ,alisema Ndahani.

Aidha amewataka maafisa maendeleo wa wilaya zote kuwasaidia vijana katika kutimiza malengo yao kwa kuwapatia mafunzo na ujuzi wa kuanzisha shughuli za kiuchumi ikiwemo usimamizi wa miradi na uandishi wa maandiko ya biashara, kilimo na ufugaji katika  maeneo yao badala ya kukaa ofisini.

Ndahani amewakikishia vijana wanawake kuwa Serikali  ya sita chini ya Rais Samia Hassan Suluhu imejipanga na   kuhakikisha inatatua changamoto zote za kiuchumi na usawa wa kijinsia kwa wanawake ikiwemo kuanzisha mifuko maalumu ya kuwawezesha wanawake ikiwemo Benki ya Wanawake na asilimia kumi ya mapato ya ndani ambayo asilimia nne huenda kwa wanawake.

Afisa huyo alisema ataendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo ya vijana ili kutimiza malengo ya serikali   ya kuwakwamua vijana katika dimbwi la umaskini katika Mkoa wa Singida.

Aidha ameishukuru Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kuratibu vizuri mafunzo hayo kwa vijana yaliyofanyika Singida na mikoa mingine katika mradi wa TIMIZA MALENGO .

Kwa upande wake Afisa Mradi wa Amref Tanzania, Mkoa wa Singida  Johnstone John Sendama amewawataka vijana hao kwenda kuwaibua na kuwasidia wasichana wote waliozaa wakiwa nyumbani ili kuwapatia mafunzo ya malezi bora ya mtoto na familia kama walivyofundishwa  ili malengo ya mradi wa TIMIZA MALENGO yaweze kufanikiwa.

Vijana walionufaika na mradi huo wameishukuru serikali na Shirika la Amref Tanzania kwa kuwaona na kuamua kuwapatia mafunzo yatakayo wasaidia katika malezi bora ya familia na watoto wao hivyo kujenga kizazi bora katika Taifa letu.

Share To:

Post A Comment: