Watendaji wakuu wa wizara, makamanda pamoja na maafisa wanaosimamia mfumo sema na Rais Mwinyi wakifutilia kwa karibu maelekezo ya Mhe. Makamu wa Pili wa Rais alioyatoa katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdull-wakili kikwajuni jijini Zanzibar.
Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said akimuahkikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa Mfumo wa Sema na Rais Mwinyi utaendelea kutatua malalamiko yanayowasilishwa na Wananchi pamoja na kuyapatia Ufumbuzi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na watendaji wakuu wa wizara, makamanda pamoja na maafisa wanaosimamia mfumo huo katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdull-wakili kikwajuni jijini Zanzibar.
MAKAMU wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka maafisa wanaosimamia mfumo wa sema na Rais Mwinyi (SNR) kuongeza kasi katika kutoa majibu ya malalamiko kutoka kwa wananchi.
Makamu wa Pili wa Rais alieleza hayo wakati akizungumza na watendaji wakuu wa wizara, makamanda pamoja na maafisa wanaosimamia mfumo huo katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdull-wakili kikwajuni jijini Zanzibar.
Mhe. Hemed aliwaeleza wasimamizi hao kuwa mfumo uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi vizuri ili lile lengo la serikali katika kuwahudumia wananchi wake liweze kufikiwa.
Alisema wananchi wamekuwa na muamko mkubwa katika kuutumia mfumo huo kwa kutuma malalamiko na changamoto zinazowakabili lakini bado kumekuwepo na changamoto ya maafisa hao kutotoa majibu kwa wakati muwafaka jambo linalosababisha usumbufu kwa wananchi kwa kuona hakuna hatua zianazochukuliwa na taasisi zinazosimamia majukumu yao.
Makamu wa Pili alisema amefurahiswa na kasi ya kiutendaji inayochukuliwa na makatibu wakuu katika kutoa ushirikiano kwa maafisa wao wanaosimamia mfumo wa sema na Rais Mwinyi (SNR) hasa katika kutatua changamoto zinazowaakabili maafisa hao akitolea mfano changamoto ya upatikanaji wa bando na vocha kwaajili ya wanasiliano.
Aidha Mhe. Hemedi alikemea vikali tabia ya baadhi ya watendaji kuwachukulia hatua watumishi wanaowasimamia wa kisingizio cha watumishi hao kutoa siri za taasisi zao kupitia mfumo wa sema na rais mwinyi
“Niseme binafsi kuchukuliwa hatua kwa watumishi wasiokuwa na nidhamu kazini lakini sitaki mtu aonewe eti kwa sababu ya kusema kupitia mfumo huu ulioaznzishwa” Alisema Mhe. Hemed
Kupitia kiako hicho makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuagiza Kamishna wa Polisi wa Zanzibar kuwasimamia kwa karibu watendaji wa jeshi hilo ambao si waaminifu wanaochukua hatua mikononi mwao ambapo ni kinyume na sharia na taratibu za Nchi.
Amefafanua kuwa, wapo askari wanaowapiga watu nyakati za usiku wakiwemo madereva na wakati mwengine abiria na kuwapa adhabu nyengine kitu ambacho ni kinyume na sheria za Nchi
Nae katibu Mkuu kiongozi na katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said alisema uwepo mfumo wa Sema Na Rais Mwinyi umekuja kurahiisisha kutatua malalamiko ya wananchi hivyo, ushirikiano wa karibu kati ya maafisa na watendaji wa taasisi wanzozisimamia unahitajika.
Mhandisi Zena alisema wananchi wanahitaji kuona tija ya mfumo huo hivyo amewahimiza maafisa hao kuwa ushirikiano wa karibu na watendaji wa taasisi ndani ya kipindi cha muda mfupi way ale malalamiko yanayowasilishwa kwao
Kwa upande wao wakuu wa taasisi walisema wamejipanga vizuri katika kuhakikisha mfumo wa sema na raisi mwinyi unafanya kazi kama ilivyokusudiwa na kuahidi kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kwa maafisa wao kwa kuwapatia mahitaji stahiki ili waweze kujibu malalamiko kwa wakati muwafaka.
Nae mtaalamu anaesimamia mfumo huo Bw. Haji Khamis Makame alisema ofisi yao imejipanga kutoa mafunzo kwa maafisa wanaosimamia mfumo huo Juni 22 na 23 kwa lengo la kuwaongezea ujuzi maafisa hao katika utendaji wao wa kazi.
Post A Comment: