MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeridhia ombi la upande wa Jamhuri la kumpeleka Mkurugenzi wa Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL), Herbinder Seth mahakamani hapo Juni 14,2021(Jumatatu) ili kuieleza mahakama hiyo mazungumzo yao na mshtakiwa yalipofikiwa.
Ombi hilo limeridhiwa na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi leo Juni 11,2021 baada ya wakili wa Serikali Mkuu, Martenus Marandu kuieleza mahakama kuwa wameshafanya mazungumzo na mshtakiwa Seth na Jumatatu wataleta mrejesho.
meeleza hayo leo Juni 11, 2021 mbele ya wakati mshtakiwa huyo (Seth) alipoletwa kwa ajili ya upande wa Jamuhuri kuleta majibu hayo.
"Mheshimiwa, mshtakiwa aliandika barua kuhusu hatma ya shauri lake Juni 10, 2021, hivyo tumekubaliana kujielekeza kwenye barua hiyo na tunaomba muda ili tuweze kuifanyia kazi na kama itakupendeza kutoa amri ya kesi hii kuja Jumatatu ili tuitaarifu mahakama makubaliano yetu yamefikia wapi.
Kufuatia taarifa hiyo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 14, mwaka huu. Mshtakiwa amerudishwa mahabusu.
Jana, (Juni 10,2021) wakili Marandu akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladslaus Komanya waliiomba mahakama kibali cha kukutana na kuzungumza na Seth ili kupata ufafanuzi juu ya barua aliyoiandika yeye binafsi na kujua kile alichokuwa amedhamiria.
Ni mshtakiwa Seth peke yake ndio ameletwa kwa ajili ya mazungumzo hayo. Huku washtakiwa wengine katika kesi hiyo, James Rugemalira ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP na Wakili wa kujitegemea, Joseph Makandege kesi yao itatajwa Juni 17, 2021.
Awali, Mahakama hiyo ilielezwaa kuwa, mazungumzo ya makubaliano ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Seth yanasuburi muongozo wa Mkurugenzi mpya wa Mashtaka nchini (DPP).
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Saimon alidai, mazunguzo ya kumaliza kesi dhidi ya mshtakiwa (Seth) yanaendelea yalipoishia, ambapo wanasuburi muongozo kutoka kwa DPP mpya aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais ili waweze kuwakilisha mahakamani hapo.
Awali Seth na Wakili wa Kujitegemea Joseph Makandege waliwasilisha ombi kwa DPP wakionesha nia yao ya kutaka maliza kesi kwa kukiri makosa yao lakini, Mei 6, 2021 mshtakiwa Makandege aliondoa nia yake ya kufanya makubaliano na DPP akieleza kwamba mazungumzo hayo yamechukua muda mrefu kukamilika.
Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 yakiwemo ya utakatishaji fedha, miongoni mwa mashtaka hayo yapo ya kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu, kughushi na kutoa nyaraka za kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Wanadaiwa kati ya Oktoba 18 ,2011 na Machi 19, 2014 jiji Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Mwanasheria Makandege, anakabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani 980,000
Post A Comment: