Madereva Bodaboda wa Halmashauri ya wilaya ya Mwanga wamemshukuru sana na kumpongeza Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Saleh Mkwizu kwa kwenda kusikiliza kero zao katika Stendi ya Mabasi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga wanapofanyia biashara zao za usafirishaji wa abiria.

Wakizungumza na Mwenyekiti huyo wamemuelezea changamoto zao na baadhi ya kero kutatuliwa hapo kwa papo.


Mkwizu amesema vijana bodaboda ni vijana wazalendo ambao wamejitafutia ajira ili wapate kipato cha halali na kuweza kuendesha familia zao pamoja na maisha yao lakini cha ajabu kazi yao haiheshimiwi wanakua wanasumbuliwa kila kukicha na migambo pamoja na askari wasio waadilifu.

"Sasa naiagiza halmashauri ya Mwanga kuwatengenezee vijana hawa mazingira rafiki ili waweze kufanya biashara vizuri."Mkwizu


"Pia ninawapiga marufuku migambo ambao wanasimamia standi hii na waache maramoja kuwasumbua vijana hawa na kuanzia leo wapaki eneo ambalo ndilo wanalolitaka na  mimi nimewakubalia kwakuwa eneo hili linawapatia wepesi wa kuwapata abiria hivyo kaeni hapa"

Hata hivyo nalipongeza Jeshi letu la polisi kwa kuendelea kuimarisha usalama wa wananchi na mali zao lakini sasa niliombe Jeshi la polisi wilaya ya Mwanga kuhakikisha linaendelea kujikita katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao  na si vinginevyo. 


"Kwani kuna baadhi ya askari polisi ambao sio waadilifu wamekuwa wakiwawinda na kuwakamata vijana hawa wa bodaboda nakuwafanya ni fursa kwao kwa kile wanachokisema eti kuwa hawafuati sheria za barabarani." Mkwizu


"Ninaomba Askari wetu watekeleze majukumu yao kwa weledi na tushirikiane kuimarisha hali ya usalama ili vijana hawa waweze kufanya biashara yao hii vizuri kwa masaa 24 wakiwa wanaimani kuwa hali ya ulinzi na usalama wa maisha yao na pikipiki zao ni salama"


"Lakini pia nitumie fursa hii kuwaeleza kuwa halmashauri  yetu ya Mwanga inatoa mikopo isiyo na riba kwa kupitia asilimia 10%  ya mapato yetu ya ndani ambopo 4% ni kwa vijana, 4% ni kwa kina mama na 2% kwa walemavu."Mkwizu


Hivyo nitoe rai kwenu vijana wenzangu muweze kuchangamkia fursa hii mujiunge kwenye vikundi vya kuanzia watu watano nakuweza kusufaika na mikopo hii isiyo na riba. Najua wengi wenu mnaendesha pikipiki za watu sasa mkiitumia fursa hii vizuri mnaweza kuendesha pikipiki zenu wenye na kuimarisha vipato vyenu maradufu kwakuwa wamilimiki mtakua ni nyie wenyewe.

Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: