Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ambaye pia ni balozi wa uhamasishaji wa mazingira katika udhibiti wa uchafuzi wa mazingira ameanza ziara za kata kwa lengo la kukagua, na kutoa elimu ya uhifadhi na ulinzi wa mazingira kwa kuhakikisha vyanzo vya maji na vya hifadhi ya mazingira vinalindwa na kuendelezwa kwa kutumia sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia na kuongoza sekta ya mazingira 


Dc Muro ambaye kwa kuanzia ameanza na kata ya Ngarenanyuki katika Kijiji cha Olkung’wado akiwa pamoja na viongozi wa Wilaya, Halmashauri pamoja na uongozi wa Kata na Kijiji ametoa maelekezo ya kuondolewa kwa mwananchi aliyekwenda kuvamia Kwenye hifadhi ya maji na kujenga kibanda pamoja na choo ambacho kinatiririsha uchafu katika chanzo kikuu cha maji kinachotumiwa na zaidi ya kata 3 za Halmashauri ya Meru


Dc Muro mbali na kutumia ziara hiyo kama sehemu ya ziara ya utoaji wa elimu na uhamasishaji wa kutunza mazingira na maeneo ya vyanzo maji amewaelekeza viongozi wa Serikali za Vijiji vyote katika Wilaya ya Arumeru kuanza mara moja zoezi la utoaji wa elimu ya mazingira kwa wananchi ambao ndio wadau wakuu wa kutunza na kulinda mazingira kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata mpaka Wilaya 


Imetolewa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru 

Share To:

msumbanews

Post A Comment: