Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Kalisti Lazaro Jana alifanya Kikao na Wazee wa Wilaya ya Lushoto Ofisini kwake na kuzungumza nao masuala mbalimbali ya Kimaendeleo Wilayani humo.
Katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya alijitambulisha kwa Wazee hao na Kuwaomba Ushirikiano katika kutekeleza Majukumu yake na Kusikiliza Kero zinazowakabili Wazee hao na kuhaidi kuzipatia Ufumbuzi kwa haraka.
Wazee hao walimueleza Mkuu wa Wilaya kuwa wanakabiliwa na Changamoto mbalimbali kama Kutokuwa na Vitambulisho, Ukosefu wa Madawa na Vifaa Tiba Mahospitalini, Kutokuwa na Bima za Afya na Kutokuwa na Madirisha Maalum ya Kutolea Huduma kwa Wazee Mahospitalini na Miundombinu ya baadhi ya Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali kutokuwa rafiki kwa Wazee.
Wazee wa Wilaya ya Lushoto wameahidi kumpa Mkuu wa Wilaya Ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake na Kumpongeza kwa kuona Umuhimu wa kukutana na Kundirika hilo Muhimu katika Jamii
Post A Comment: