Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo akizungumza katika Mkutano Maalumu na Waendesha Mabasi, Daladala, Bajaji na Bodaboda uliofanyika leo jijini Arusha huku changamoto mbalimbali zilijadiliwa na kupatiwa ufumbuzi.
Serikali imewaasa madereva wa bodaboda nchini kutoshiriki matendo ya uhalifu ikiwemo usafirishaji wa wahamiaji haramu,dawa za kulevya,mauaji na uporaji wa vitu mbalimbali huku ikisisitiza atakayematwa akishiriki matendo hayo atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
“Nawaasa bodaboda kuachana na matendo ya kihalifu,serikali tunawategemea sana vijana kama nguvu kazi lakini kuna baadhi ya vijana sio wote wanatumika katika matukio ya uhalifu ikiwemo ujambazi,dawa za kulevya na wengine wakitumika huko mipakani kusafirisha wahamiaji haramu sasa tusizitumie bodaboda zikaleta sura mbaya kama chombo cha kutumika kufanya uhalifu wakati lengo lake ni kutumika kujikwamua kiuchumi” alisema Naibu Waziri Khamis Hamza Chilo
Akizungumza katika Mkutano huo Mbunge wa Arusha Mjini,Mrisho Gambo amewaomba bodaboda kutii sheria za usalama barabarani huku wakisubiri mapendekezo ya Bunge kuhusiana na kila kosa kutozwa Shilingi Elfu Kumi yapitishwe
“Serikali imesikia kilio chenu cha muda mrefu cha kushushiwa gharama ya faini kutokana na makosa ya barabarani tunamshukuru Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kusikia kilio chenu nawaomba sasa mfuate sheria za usalama barabarani mkishirikiana na Jeshi la Polisi” alisema Gambo
Kwa upande wake Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamanda wa Polisi Mmoa wa Arusha.Kamishna Msaidizi wa Polisi Justine Maseji amewaonya watu wanaoshiriki matendo ya kuteka na kuwaua madereva bodaboda huku likionya kwa yoyote anayejaribu kucheza na Maisha ya watanzania kushughulikiwa ipasavyo.
“Mpaka mwezi wa tatu tumekamata pikipiki sitini,nitoe onyo kali kwa watu wanaopora mali za wananchi waache kufanya mambo ya ovyo ovyo tutachukua hatua kali,mtu anayetafuta dozi sisi tutapeleka dozi kali zaidi na wao wahalifu wanafahamu maana sio kila kitu tunaweka wazi wanazijua ‘sindano’ tunazopeleka”alisema ACP.
Post A Comment: