Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (katikati aliyevaa kofia) akimsikiliza Afisa Usajili kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na (BRELA), Gabriel Girangay akilipo kuwa akimuelezea jitihada wanazofanya za kuboresha huduma zao wanazotoa kwa wananchi alipotembelea Banda la maonesho la BRELA katika Viwanja vya Rock City Mall, Jijini Mwanza tarehe 1 Mei, 2021. Kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba na kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Utalii yanayofanyika katika katika Viwanja vya Rock City Mall, Jijini Mwanza jana. Kushoto kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango,  Dkt. Mwigulu Nchemba, kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja akifuatiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Godfrey Nyaisa.


Maofisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wakihudumia wadau mbalimbali waliofika katika banda lao katika maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Utalii kwenye Viwanja vya Rock City Mall, Jijini Mwanza jana.

Maofisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wakihudumia wadau mbalimbali waliofika katika banda lao katika maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Utalii kwenye Viwanja vya Rock City Mall, Jijini Mwanza jana.


 Kikao kikiendelea



Na Mwandishi Wetu, Mwanza


WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki aliyekuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Utalii, amefurahishwa na utendaji kazi Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Ndaki alionesha kufurahishwa na hatua hiyo  ya utendaji kazi wa  taasisi hiyo  alipotembelea Banda lao la maonesho katika Viwanja vya Rock City Mall, Jijini Mwanza  jana.

Afisa Usajili kutoka Brela,  Gabriel  Girangay akielezea mafanikio ya taasisi hiyo alisema imeboresha huduma inazotoa kwa wadau wake ikiwa  ni pamoja na kupunguza muda wa kukamilisha usajili kwa kadri inavyowezekana lakini pia kuwahudumia wateja wote kwa ukaribu kupitia kituo cha miito.

“Kwa sasa muda wa usajili wa jina la biashara ni siku moja (1) na si zaidi ya siku tatu (3) za kazi, Usajili wa kampuni ni siku tatu (3) na si zaidi ya siku tano (5) za kazi. Usajili wa Alama za Biashara na huduma ni kipindi cha siku tisini (90) (kutokana na takwa la kisheria).

Maombi ya kupata Hataza ni siku mia moja na ishirini (120) (kutokana na takwa la kisheria), kupata Leseni ya Kiwanda au Leseni ya Biashara kundi A ni siku moja (1) na si zaidi ya siku tatu (3) za kazi”. alibainisha  Girangay.

Aidha, akisoma hotuba  ya ufunguzi wa maonesho hayo  Ndaki amewataka wafanyabiashara na wajasiriamali wa Mkoa wa Mwaza kutumia fursa ya uwepo wa taasisi hiyo katika maonesho hayo kutatua changamoto zao na kupata elimu.

“Changamoto zinazosemekana zipo katika urasimishaji biashara sasa ndio muda wake kuzimaliza na bahati nzuri Brela wapo katika maonesho haya, fikeni katika banda lao la maonesho, pateni elimu, wasilisheni changamoto zenu hapo na rasimisheni biashara papo kwa hapo”. alisema Mhe. Ndaki.

Brela inashiriki maonesho haya ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kuwafikia wadau wake katika maeneo yao kwa lengo la kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kurasimisha biashara, taratibu za urasimishaji biashara na gharama zake, kutatua changamoto na kufanya usajili wa papo kwa hapo.

Maonesho ya Biashara Uwekezaji yanafanyika kwa siku tatu kuanzia Aprili 30 hadi  leo.

Share To:

Post A Comment: