Viongozi wa Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma na Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina |
Sehemu ya baadhi ya wanavyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakifuatilia mjadala wa hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto bungeni Dodoma.
Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu mbalimbali nchini wanaotoka Jimbo
la Kisesa wamefika bungeni kujifunza namna Bunge linavyoendesha shughuli
zake huku wakiahidi kusoma kwa bidii ili waweze kutoa mchango
unaostahili kwa jimbo lao na Taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti
wa Umoja wa wanafunzi wa vyuo kutoka Jimbo la Kisesa, Ndugu Sitta
Kuzenza Nyangwakwa amesema umoja huo umeanzishwa kwa lengo la
kuwakutanisha pamoja vijana wote wanaosoma vyuo mbalimbali kuanzia ngazi
ya Diploma hadi Digrii wanaotoka Jimbo la KIsesa.
Amesema
tayari wanafunzi wa vyuo wanaotoka Jimbo la Kisesa kutoka Mikoa ya
Dodoma, Morogoro, Dar es Salaam, Mbeya wanaendelea kujiunga ili kuunga
mkono juhudi za Serikali pamoja na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina
katika kuwaletea maendeleo ya jimbo hilo huku akitumia nafasi hiyo
kuwahamasisha vijana wengine wanaotoka Jimbo la Kisesa kujiunga na umoja
huo.
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo kutoka Jimbo la Kisesa wakiwa katika viwanja vya Bunge na Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina |
Post A Comment: