Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida Dkt.Denis Nyiraha, akizungumza na vijana wa chama hicho wa Wilaya ya Iramba baada ya kuanza ziara ya kikazi na kamati ya utekelezaji jana.
Ziara ikiendelea.
Safari ya kuelekea kukagua miradi ya maendeleo ikifanyika.
Na Mwandishi Wetu, Iramba
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida Dkt.Denis Nyiraha ameiomba Serikali kutoa kwa wakati gawio la asilimia nne kwa vijana.
Nyiraha alitoa ombi hilo jana wakati alipokuwa na Kamati ya utekelezaji katika ziara ya kikazi wilayani Iramba ambapo walitembelea vikundi viwili vya vijana vilivyonufaika na asilimia 4 ya mkopo kutoka halmashauri.
"Naiomba Serikali itoe gawio
hilo wa wakati na kwa mgao sawa ili iweze kuwa daraja la maendeleo kwa vijana wetu na kwa taifa zima."alisema Nyiraha.
Wajumbe wa kamati hiyo pia
walikagua ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM wilayani humo na kuitaka kamati ya ujenzi kumaliza haraka jengo hilo.
"Haya na mimi natoa hii laki moja kwa ajili ya kuchangia juhudi za kumalizia jengo hili pia nawaomba watu wote walio toa ahadi basi wamalizie kutoa kwa wakati ili tufikie malengo yetu." alisema Nyiraha.
Katika hatua nyingine Dkt.Nyiraha alifanya vikao vya ndani lengo likiwa kukagua uhai wa jumuiya na chama katika Kata ya Kiomboi, Ulemo na Kata Ya Kyengege.
Wakiongea kwa nyakati tofauti viongozi wa vikundi vya vijana walio patiwa mikopo ya asilimia 4. kutoka halmashauri wameushukuru umoja wa UVCCM kwa kuwapigania na kuwaweka pamoja na kuwa na uwezo wa kukopesheka bila vikwazo.
Kamati hiyo ya utekelezaji chini ya Dkt.Nyiraha leo itaendelea na ziara hiyo Singida mjini.
Post A Comment: