“Tumezindua simu ya kisasa zaidi ‘Infinix Hot 10t’ kwenye soko letu la Tanzania na sasa wateja wetu kote nchini wataweza kupata mtandao wa 4G kwa kupitia simu hizi”. Mkumbo Muyonga-Meneja wa bidhaa za intaneti Tigo |
Meneja wa bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Muyonga alisema “Katika mkakati wetu wa kuchochea matumizi ya simu janja na mtandao wa 4G nchini, tunaendelea kuungana na Infinix Tanzania ili kuhakikisha wateja wetu na watanzania wote wanapata simu zenye uwezo wa 4G”.
Aliongeza “Leo tumezindua simu ya kisasa zaidi ‘Infinix Hot 10t’ kwenye soko letu la Tanzania na sasa wateja wetu kote nchini wataweza kupata mtandao wa 4G kwa kupitia simu hizi”.
Myonga aliongeza kuwa uzinduzi wa simu ya Infinix Hot 10t kwenye soko la Tazania utaongeza thamani ya biashara na pia kuboresha maisha ya watanzania wengi.
“Kwa kuongeza na kuhakikisha wateja wanapata huduma bora zaidi kwa gharama nafuu, simu hii ya Infinix Hot 10t itasaidia katika kuongeza idaidi ya watumiaji wa simu janja nchini.”
Kwa mujibu wa Myonga “Simu hii itapatikana katika maduka yote ya Tigo nchini na inakuja ikiwa na kifurudhi cha GB 78 kwa mwaka mzima bure.”
Ofisa Mahusiano wa Infinix alisema “Simu ya Infinix Hot 10t inakuja na kadi maalumu ya Helio G70 inayoiwezesha simu kuwa na uwezo mkubwa kwenye games, betri yenye uwezo wa 5000Ah inayoweza kukaa masaa 24 ukiwa umewasha data.”
Infinix Hot 10t ina nchi 6.82 na 90hz muonekano maridadi wa kioo ambao unampa mtumiaji uhuru wa kutazama video na picha zilizopigwa na camera yenye Ai portrait. Simu ya Hot 10t inapatikana katika maduka yote ya Infinix na Tigo nchi nzima.”
Post A Comment: