Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel
|
Mlezi wa TAMUFO, Frank Richard
Na Dotto Mwaibale
UMOJA wa Wanamuziki Tanzania
(TAMUFO) unaratajia kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Makumbusho Duniani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa juzi Katibu
Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel alisema tayari wanamuziki kadhaa wameonesha nia ya
kuadhimisha siku hiyo.
" Baadhi ya wanamuziki wameonesha nia ya kuhudhuria
maadhimisho hayo ya makumbusho ya Taifa yatakayofanyika Mei 18, 2021."
alisema Joel.
Mlezi wa TAMUFO, Frank Richard alisema muziki ni sehemu katika
Kuadhimisha Siku ya Makumbusho Duniani.
" Muziki ni wa muhimu sana hasa katika kipindi hiki
ambacho tunahamasisha uanzishwaji wa makumbusho mbalimbali hapa nchini zikiwemo za Wanamuziki kama mataifa mengine
yaliyoendelea yanavyofanya.
Richard alisema nchi
nyingi duniani zina makumbusho mbalimbali zikiwemo za wanamuziki hivyo umefika
wakati kwa wanamuziki wa Tanzania kupata
elimu kuhusu makumbusho ili waweze kuzianzisha chini ya taratibu na sheria za
nchi. |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Back To Top
|
Post A Comment: