Viongozi wa REPSSI Tanzania wakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Kanoni Lauteli  (kushoto) kabla ya kuanza mafunzo.

Viongozi wa REPSSI Tanzania wakiwa nje ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe.


       Kamati ya ulinzi na usalama ya mama na mtoto, Wilayani Wanging'ombe wakiwa katika picha baada ya mafunzo..
Mafunzo yakitolewa na shirika hilo.
Mafunzo yakitolewa na shirika hilo.
Mafunzo yakiendelea.
 


Na Mwandishi Wetu, Njombe


SHIRIKA  la Regional Psychosocial Support Initiative (REPSSI) kwa kushirikiana na Tamisemi limetoa mafunzo juu ya namna ya kutoa msaada wa kisaikolojia kwa jamii, wakati wa majanga.

Mafunzo hayo yaliyotolewa kwenye mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya yamezishirikisha kamati za ulinzi na usalama za mama na mtoto katika kila halmashauri kwenye mikoa hiyo.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa REPSSI Tanzania, Edwick Mapalala amesema licha ya huduma nyingi ambayo huwa zinatolewa kwenye majanga kama moto, mafuriko, ajali na mengine, msaada wa kisaikolojia ni muhimu.

Amesema wanawake, watoto na watu wenye ulemavu huwa wahanga zaidi wa majanga hayo hiyo mafunzo yaliyotolewa yanaziandaa kamati husika kuweza kutoa msaada huo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Kanoni Luteni ameshukuru mafunzo hayo na kwamba, msaada wa kisaikolojia ni muhimu kutolewa kwa kila jamii.

Mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo, kamati hizo zilifanikiwa kuandaa mpangokazi wa kila halmashauri katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Share To:

Post A Comment: