Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof.Shadrack Mwakalila leo ametembelea banda la Chuo hicho la maonesho ya Kitaifa ya Sayansi Teknlojia na Ubunifu (MAKISATU - 2021) na kusema kuwa Chuo kimejikita katika kutoa kozi mbalimbali ambazo zinawajengea uwezo wanafunzi wabunifu kupata maarifa na kuwa bora zaidi.


Akizungumza na waandishi wa Habari mkoani Dodoma hii leo Prof. Mwakalila amesema lengo la ubunifu ni kuwajengea uwezo vijana kuendeleza ubunifu wao ili kuingia kwenye soko la ajira, kuajiri wengine na kuendeleza ujasiriamali.


Kauli Mbiu ya Maonesho hayo kwa Mwaka huu ni Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kwa Uchumi Endelevu.


Imetolewa na :


Kitengo Cha Habari na Mahusiano

MNMA

07.05.2021







Share To:

msumbanews

Post A Comment: