Waziri wa Elimu Sayansi naTeknolojia Prof. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wake na viongozi wengine wakimuangalia Mbunifu wa FARM CUT kutoka SUA, Mussa Dotto akionyesha matrekta shamba hilo linavyofanyakaz iwakati wa MAKISATU 2021 Dodoma.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo akitoa maelezo ya mashindano hayo ya MAKISATU 2021 kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua maonesho na mashindano hayo jijini Dodoma.
Wananchi wakimiminika kwenye banda la SUA kuangalia bunifu na teknolojia mbalimbali ambazo wamekuja kuzionyesha kwenye maonesho hayo ya MAKISATU 2021 Jijini Dodoma.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda akiwa kwenye picha ya pamoja na waonyeshaji kutoka SUA Kwenye banda la SUA lililopo kwenye maonesho ya MAKISATU 2021 jijini Dodoma.
Fundi sanifu wa maabara ya Kemia na Fizikia SUA, Anneth Coster akiwaonyesha Wanafunzi namna Indicator iliyozalishwa na SUA kwa ajili ya somo la kemia kwa wanafunzi wa shule za sekondari.
Na Calvin Gwabara - Dodoma
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa jitihada wanazozifanya katika kuibua Wabunifu,Teknolojia na mbinu zingine za kisayansi pamoja na kuwa saidia na kuendeleza wabunifu hao ili waweze kufikia ndoto zao na kusaidia jamii na taifa.
Pongezi hizo ametoa wakati akitembelea kukagua kazi za wabunifu wa SUA na maonesho yao kabla ya kuzindua rasmi mashindano ya kitaifa ya sayansi,teknolojia na ubunifu (MAKISATU 2021) jijini Dodoma yanayokutanisha wabunifu kutoka nchi nzima kwenye makundi saba ya ushindani.
Akizungumza wakati akifungua mashindano hayo amesema kuwa miongoni mwa mafanikio ambayo Serikali imeyapata katika kuendeleza Sayansi na Ubunifu nchini ni pamoja na kuibua na kutambua wabunifu wachanga 1066 kupitia MAKISATU 2019/2020 ambapo kati ya hao wabunifu mahiri 130 wanaendelezwa na Serikali ili bunifu zao zifikie hatua ya kubihasharishwa na hivyo kuongeza fursa za ajira kwa vijana na kuchangia kwenye pato la taifa.
“Ni matumaini na matarajio yangu kuwa bidhaa zinazozalishwa na wabunifu na wavumbuzi nchini zitaongeza tija katika uzalishaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda na kuongeza thamani ya bidhaa zinazo zalishwa pamoja na kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma katika Nyanja mbalimbali” Alisisitiza Prof. Ndalichako.
Aidha Prof. Ndalichako ameeleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2015 hadi mwaka 2020 Serikali imefadhili jumla ya miradi 215 ya sayansi teknolojia na ubunifu kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo na Mifugo, Afya, Nishati, Maliasili na Viwanda aidha kupitia mfuko wa taifa wa uendelezaji Sayansi naTeknilojia Serikali imewajengea uwezo watafiti 579 katika masomo ya uzamili na uzamivu ili kuwaongezea weledi kwenye utafiti.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi huyo kufungua maonesho hayo ya MAKISATU 2021Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt.Leonard Akwilapo amesema mashindano hayo ya MAKISATU yalianzishwa mwaka 2019 yakiwa ni moja ya mikakati ya Wizara ya kuibu,kutambua na kuendeleza bunifu na vumbuzi zinazofanywa na Watanzania na kukuza hamasa ya ubunifu na kuhamasisha matumizi ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu katika shughuli ya kijamii na kiuchumi utakaotegemeza maendeleo ya uchumi wa viwanda.
Amefafanua kuwa katika kipindi cha miaka miwili ya MAKISATU jumla ya wabunifu 1066 waliibuliwa na kutambuliwa na Wizara na wabunifu mahiri 130 wanaendelezwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi naTeknolojia (COSTECH) ili ubunifu wao ufikie kubiasharishwa na hivyo kuongeza fursa za ajira kwa vijana.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof.Raphael Chibunda alimwambia Waziri huyo kuwa katika kuhakikisha wabunifu wa SUA wanafikia hatua za kubihasharisha wanatarajia kumpatia kiasi cha shilingi milioni 20 mmoja wa wabunifu wao Mussa Dotto aliyebuni Trekta la kulimia aliloliita FARM CUT ili aweze kuzalisha matrekta hayo matatu yaingie sokoini.
Amesema walipoonaamebuni trekta hilo waliamua kumsaidia kupitia mfuko wa ubunifu wa Chuo lakini lengo lingine ni kutaka kuwaonyesha wanaosema elimu imeshuka waone namna ambavyo vijana wanawezakufanya mambo makubwa vyuoni na kunufaika pamoja na kunufaisha jamii na taifa.
Chuo Kikuu cha Sokone cha Kilimo SUA kinashiriki maonesho hayo kwa kuonyesha kazi zake mbalimbali za kitafiti na kibunifu lakini pia kimeingiza Wabunifu watatu kwenyemashindano hayo ya MAKISATU kupitia kundi la vyuo vikuu ambalo lina wabunifu 10.
Kauli mbiu ya mwaka huu inasema Sayansi Teknolojia na Ubunifu kwa Uchumi Endelevu.
Post A Comment: