_Na Mwandishi Maalum_
Leo tarehe 24 Mei, 2021 Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akiwa ameambatana na Kamishna wa Tume ya Madini, Janeth Reuben Lekashingo wametembelea Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi na Ofisi ya Madini ya Kahama lengo likiwa ni kuangalia shughuli za uchimbaji wa madini na kutatua changamoto mbalimbali.
Akiwa katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Kahama kupitia kikao chake na watumishi wa ofisi hiyo, Profesa Kikula ameipongeza ofisi kwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka wa fedha 2020-2021 ambapo mpaka sasa ofisi imekusanya kiasi cha shilingi bilioni 82 ambazo ni sawa asilimia 103.4 ya lengo lilikowekwa la shilingi bilioni 79.
Amewataka watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana, kujituma na kuendelea kuibua vyanzo mbalimbali vya maduhuli ili kuiwezesha Tume ya Madini kufikia lengo la makusanyo ya Bilioni 650 kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Katika hatua nyingine Profesa Kikula amesema kuwa Tume itaendelea kutatua changamoto za watumishi na kuwawezesha ili wafanye kazi katika mazingira bora zaidi.
Post A Comment: