|
Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Profesa Henry Mahoo,
akizungumza na Menejimenti ya Ofisi hiyo, (haipo pichani) katika makao
Makuu ya Ofisi hiyo jijini Dodoma jana jioni. |
|
Kushoto Profesha Henry Mahoo, akimsikiliza Mhaandisi Hassan Dyali
alipokuwa akitoa maelezo kuhusu mitambo inayomilikiwa na Tume ya Taifa
ya Umwagiliaji. |
|
Picha ikionesha sehemu ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
walipokuwa wakimsiliza Mwenyekiti wa Bodi katika kikao jana jioni. |
Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Profesa, Henry Fatael Mahoo, ameitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kujikita zaidi katika kutoa elimu kuhusu kilimo shadidi cha mpunga alichoeleza kuwa kinaweza kuongeza Tija katika sekta hiyo.
Profesa Mahoo, ameyasema hayo Jijini Dodoma jana Jioni alipokutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Alisema kilimo hicho kinaweza kuleta Tija kwa kuongeza uzalishaji wa Tani saba(7) mpakakumi (10) kwa hekta katika miradi ya kilimo cha umwagiliaji yenye uhakika wa maji.
“Tutakuwa tunatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2020 – 2025 yakufikia malengo yaongezeko la chakula.” Alisisitiza Profesa.
Sambamba na hilo, Mwenyekiti huyo wa Bodi aliitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuwajengea uwezo wataalam wake wa ndani pamoja na wakulima ili kuweza kwenda sambamba na matumizi sahihi ya teknolojia ya kisasa katika sekta ya kilimo cha Umwagiliji.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali amesema kuwa,Tume inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Kilimo cha umwagiliaji nchini ambapo kwasasa imejikita katika kuboresha na kujenga miradi ya ujenzi shirikishi ambayo haijakamilika.
Aidha aliongeza kwa kusema kuwa,uzalishaji wa zao la mpunga umeongezeka kwenye maeneo ya kilimo cha umwagiliaji kutoka tani laki saba na kumi na nneelfu (714,000) toka mwaka 1989/1990/2000 hadi kufikia tani milioni mbili na elfu tisa na miambili sabini na nne (2,009,274) mwaka 2018/2019.
Post A Comment: