Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida Dkt. Denis Nyiraha (katikati mwenye shati la njano) na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wakikagua ujenzi wa nyumba ya Katibu wa umoja huo mkoani hapa jana.




Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida Dkt. Denis Nyiraha (katikati mwenye shati la njano) na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wakisalimiana na wafanyabiashara waliopanga kwenye vibanda vya umoja huo Stendi Mpya ya Mabasi Misuna mkoani hapa.

Ukaguzi wa vibanda ukifanyika.
Kikao na wafanyabiashara kikifanyika.


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida Dkt. Denis Nyiraha (katikati mwenye shati la njano) na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wakikagua jengo la Hosteli la umoja huo.
 


Na Dotto Mwaibale, Singida.


 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida Dkt. Denis Nyiraha na Kamati ya Utekelezaji jana   wameendelea  na ziara ya kikazi na kukagua ujenzi wa nyumba ya umoja huo mkoani hapa ambapo alichangia Sh.500,000.

Dkt. Nyiraha amechangia fedha hizo ili zisaidie kuwekea madirisha na milango ya nyumba hiyo iliyopo eneo la Stendi Mpya ya Misuna mjini hapa.

Mbali ya kukagua ujenzi wa nyumba hiyo  kamati hiyo pia ilikagua jengo la Hosteli la vyumba 18 linalo jengwa kwa ajili ya uwekezaji ambapo pia walikagua ulipaji wa kodi katika vibanda 150 vilivyo kodishwa.

Akizungumzia ziara hiyo Dkt.Nyiraha alisema mbali ya kukagua vibanda hivyo waliangalia uwezekano wa kukamilisha ujenzi wa vibanda.vingine 34 vilivyo katika hatua ya ujenzi.

Baada ya ukaguzi wa miradi hiyo mwenyekiti huyo na kamati hiyo ya utekelezaji walizungumza na wafanya biashara waliopanga kwenye vibanda hivyo ili kujua changamoto zao.

Moja ya changamoto kubwa waliyoiibua ni kutokuwepo kwa miundombinu ya barabara ya kwenda kwenye vibanda hivyo.

Baada ya kupokea changamoto hiyo Dkt.Nyiraha aliwasiliana kwa njia ya simu na viongozi wa Serikali wa wilaya ya Singida mjini ambao walitoa ahadi wiki ijayo kuanza kuifanyia ukarabati barabara hiyo chini ya Wakala wa Barabara za Vijijini na  Mjini  ( TARURA)

Wafanyabiashara hao wakizungumza katika kikao hicho wameaiomba jumuiya hiyo ya vijana wa CCM kuwajengea miundombinu hiyo ambapo walitoa ahadi ya kulipa kodi kwa wakati.


Share To:

Post A Comment: