NA MWANDISHI WETU, ARUSHA
WAKULIMA wa mazao mchanganyoko katika mikoani ya Manyara na Arusha wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan (SSH) kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza mwanamke wa CCM Taifa, wakimshauri kutengua kitendawili kuhusu kiwanda cha unga cha NMC Arusha.
Aidha, wakulima hao wamepongeza hatua ya kuchaguliwa kwa Sekretarieti mpya, inayoongozwa na Katibu Mkuu mpya, Daniel Chongolo, wakisema hatua hiyo inarejesha Imani kwa wanaCCM na wananchi kwa ujumla waked na matumaini mapya.
Wakizungumza na gazeti hili, wakulima hao walisema kuchagukua kwake, kama kiongozi wan chi na mwenyekiti wa chama, kumewafanya watambue uhakali wake wa kisera na kiilani, kurejesha matumainii ya wakulima kwa kutengua utata uliochukuliwa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, kufunga kiwanda hicho cha Unga NMC.
Kiwanda hicho ambacho awali kilikuwa sehemu ya mali za lililokuwa Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC), kilibinafsishwa mwaka 2007 chini ya Shirika la Hodhi ya Mali za Serikali (CHC), kwa kampuni ya kizalendo ya MONABAN Trading and Farming Limited.
Hatua hiyo ya CHC ililenga kukifufua kiwanda hicho na kuanza tena uzalishaji, kwa nia ya kusaidia wakulima wa mazao kama maihindi na ngano kwa mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga, ambao, walionekana kukosa soko la uhakika na mwekezaji huyo alielekezwa kuongeza ufanisi na kuwafikia wakulima wengi na hasa wanaozungumza mkoa hiyo
Hata hivyo, ilibainika kuwa maamuzi ya bodi hiyo chini ya mama Monica Mbega, kufunga kiwanda hicho, ili kuruhusu kuanza uota kwa mchakato yameathiri ajira zaidi ya 1,000 za watu waliokuwa wameajiriwa kiwandani hapo na wategemezi wao zaidi ya 4000 wakibaki midomo wazi.
Kulingana na wakulima hao, hatua ya kufungwa kwa kiwanda hicho kwa miaka mitatu na nusu sasa, huku jamii ikishindwa kuelezwa maana halisi ya sera na ilani ya CCM katika uendelezaji wa sekta ya kilimo mkoani Arusha.
Aidha, uamuzi wa bodi umeendelea kulalamikiwa na wakulima hao kwenye, ambao sasa wameamua kufikisha kilio hicho kwa Rais, aliyekabidhiwa kijiti cha uongozi wa nchi na chama, kutumia mamlaka yake ya kikatiba kuchukua hatua za haraka kutafutia ufumbuzi sahihi wa jambo hilo.
Wananchi hao wamedai kuwa kusitishwa kwa shughuli za uzalishaji za kiwanda hicho, kumewaumiza wakulima wengi, lakini kulichangiwa na mashinikizo ya baadhi ya viongozi waandamizi serikalini, pamoja na vita ya kisiasa mkoani Arusha.
Wakulima hao wamedai hatua ya bodi ilikifunga kiwanda hicho Juni mwaka 2018, mbali na kuathiri wananchi wengi kiuchumi, ilikuwa na nia ya kumdhibiti mmiliki wa kampuni ya Monaban Trading and Farming Limited, kugombea Ubunge katika Jimbo hilo la Arusha.
“Tumeamua kumuomba Rais, kuchukua hatua kulitafutia ufumbuzi jambo hili, siasa zisichangie umasikini, tumefunga kiwanda, uchaguzi umekwisha lakini kwa sasa hakuna kitu kinachoendelea, hakuna mchakato na ajira zaidi ya 1000 zimepata shida” alisema Mkolongwa Mwatibu, mkulima wa ngano wilyani Babati mkoa wa Manyara.
Mwatibu aliongeza kusema, suala hilo lilifikishwa kwa Hayati Rais Magufuli, wakati akiwa katika kampeni za uchaguzi mkuu, lakini pia wadaui wa klilimo wa mikoa hiyo, walimfikishia Rais Samia, wakati akiwa mgombea mwenza, hivyo sio suala geni masikioni mwake.
Mkulima Matrida Koisela, aliongeza kusema kuwa hatua ya kufungwa kwa kiwanda hicho, kulifanywa kwa chuki na uonevu, kumewafanya wakulima kupoteza soko la uhakika la mazao yao.
“tunaamini kuwa Rais Samia, ameletwa na Mungu, kutafuta Haki na Aamani ya wat una hasa walionewa, ili kulifanya Taifa kuwa na Umoja na mshikamano, lakini sio kwa hali kama hii, watu wanaonewa hadharani, huku tunaimba amani na upendo sio,” alisema Mama Matrida Koisela.
Mama Koisela, mkazi wa Ngarenalo Jijini Arusha, alisema vijana 1000 waliopoteza kazi kwenye kiwanda hicho, wengi wao wakiwa ni makada wa CCM, na kutokana na maamuzi hayo walifikia hatua ya kutaka kuinyima kura CCM, wakiamini kuwa ni muendelezo wa mateso kutoka kiwandani mpaka kwenye ubunge.
“Vijana wana hasira, mitaani wanasema hadharani, Gambo ameshiriki kufungwa kwa kiwanda ambacho wao walikuwa wakipata mkate wao wa kila siku, leo CCM imemleta Gambo kugombea katika jimbo hilo,” alisema Mama Koisela.
Wakulima hao walisema kuwa, “Kwa sasa kauli Rais Magufuli, ndio inayosubiriwa na wengi na hasa wananchi wa Jiji la Arusha, kuhusu uhalali wa kufungwa kwa kiwanda hicho, ama kufunguliwa na kurejesha imani kwa watu wengi walioumizwa na jambo hilo,” walisema wakulima hao
Kwa mujibu wa wananchi, Mwekezaji aliyenyang’anywa kwa hila za wakubwa kiwanda hicho, aliwekeza zaidi ya Bilioni 13, kufufua kiwanda hicho ikiwa ni pampja na kazi ya kutengeneza kinu cha kukoboa na kusaga unga wa ngano na mitambo mingine mikubwa iliyokuwa imekufa.
“Huu ni uwekezaji mkubwa, tena umefanywa na mtanzania mzalendo, jambo hli halipaswi, kuachwa likapita hivi hivi, lakini imani yetu, muhusika na mwenye maamuzi ya mwisho ni Rais Samia,” walisema na kuongeza kuwa wapo watu wanopenyeza fedha kuhujumu mikakati ya kumsaisia mkulima mnyonge.
Waziri wa Kilimo, Profesa Mkenda, hakuweza kupatikana kuzungumzia jambo hilo kutokana na kutopatikana kwa simu yake ya kiganjani, lakini pia
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, Mama Monica Mbega, hakuwa tayari kulizungumza suala hilo, japo kuwa alisema anafahamu kufungwa kwa kiwanda hicho, ili kupisha mchakato.
Alipotakiwa kueleza mchakato huo unachukua muda gani na kama kuna manufaa kufunga kiwanda na kupoteza soko la uhakika la mazao ya wakulima na ajira za watu wengi, hakuweza kutoa majibu.
Uchunguzi wa gazeti hili, umebaini kuwapo kwa mkakati wa kiwanda hicho kupewa mfanyabiashara mwenye asili ya Asia, anayedaiwa pia kuwa mshirika wa karibu wa mwanasiasa mmoja mkoani Arusha.
Post A Comment: