Na,Jusline Marco;Arusha
Naibu waziri wa wizara ya katiba na sheria Geoffrey Mizengo Pinda amewataka wananchi na viongozi wote kutambia kuwa takwimu sahihi za vizazi ni kichocheo kikubwa cha uchumi katika nchi kwani itasaidia serikali kupanga mipango yake ya maendeleo kwa usahihi.
Akizindua mpango wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka mitano kwa mikoa ya Arusha na Manyara ,Pinda alisema katika sensa ya mwaka 2012 asilimia 13.4 tuu ya watanzania ndio WALIOKUWA wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa.
Adha ametoa wito kwa mikoa yote nchini ambayo imeshafikiwa na zoezi hilo kuhakikisha wanaendelea kusajili kwani kila siku watoto wanazaliwa ikiwa ni pamoja na kuutaka mkoa wa Arusha na Manyara kuingia katika ushindani wa zoezi hilo na itakapofika wakati wa tathimini kila mmoja awe ametoa alipo na kuwa juu.
Naye mwenyekiti wa bodi ya RITA Prof Hamis Bihenga alisema kuwa wapo katika mikakati wa kuhakikisha kuwa matukio tote muhimu ya binadamu ikiwemo kuzaliwa yanasajiliwa kwani kwa kufanya usajili huo serikali itajua idadi ya watoto wote waliozaliwa na baada ya miaka saba wanahitaji kwenda shule hivyo itasaidia kuondoa changamoto mbalimbali ikiwemo ya madarasa na madawati.
Amesema kuwa zoezi hilo kwasasa linafanyika katika ofisi za kata na katika maeneo yote panapotolewa huduma ya mama na mtoto ili kuondoa mrundikano wa watu wasio kuwa na vyeti vya kuzaliwa hapo baade ambapo usajili kwa sasa asilimia 13.4 na wanatarajia kufikia asilimia 55 huku lengo likiwa kufikia asilimia 100.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akimwakilisha mkuu wa wa mkoa Arusha Iddy Kimanta amesema kuwa wananchi wengi mpaka sasa hawajasajiliwa na ndio maana takwimu kwa mkoa wa Arusha zipo chini lakini kwa kuanza kwa utekelezaji huo na kuweza kupata takwimu sahihi hivyo wilaya na halmashauri zote zihakikishe zoezi hilo linafanikiwa kwa asilimi 100.
Naye mkuu wa mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti alisema kuwa changamoto kubwa iliyopelekea mkoa wake kuwa chini katika usajili ni pamoja na ukubwa wa mkoa huo kwani kutoka kata moja kwenda kata nyingine ni sawa na kutembea wilaya nzima ya mikoa mingine ambapo pamoja na changamoto hiyo watahakikisha kuwa zoezi hilo linafanikiwa.
Post A Comment: