Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara akifungua mkutano wa mashauriano na wadau wa sekta ya ujenzi kwa mwaka 2021,uliofanyika jijini Arusha.
Wakandarasi walioshiriki mkutano wa mashauriano na wadau wa sekta ya ujenzi kwa mwaka 2021 wakifuatilia hotuba ya Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi Mhe.Mwita Waitara.

 Na,Jusline Marco;Arusha


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mwita Waitara amesema kuwa serikali inaendelea kushirikiana na bodi ya usajili wa makandarasi katika kuhakikisha jitihada za uongozi wa makandarasi wa ndani zinafanikiwa.


Akifungua mkutano wa mashauriano na wadau wa sekta ya ujenzi kwa mwaka 2021,wenye kauli mbiu ya JUHUDI ZA MAKUSUDI ZA WADAU KUWEZESHA UKUAJI WA MAKANDARASI WA NDANI" Mhe.Waitara alisema kupitia miradi mikubwa miwili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Ulamno hadi Kaliuwa wenye kilometa 28 na Ludewa Kilosa wenye kilometa 24 ulitengwa mahususi kwa ajili ya maknsarasi wazawa.


Aidha alisema kuwa serikali inaahidi kuendelea kutenga miradi mahususi lwa makandarasi wa ndani kama sehemu ya ustawi wa kuwaweka pamoja makandarasi ili kuongeza uwezo wa makandarasi wa ndani sambamba na kuweka vigezo na masharti nafuu yatakayotoa mazingira rafiki kwa ukuwaji wa makandarasi.


Vilevile alisema serikali itaendelea kusimamia matakwa ya kisheria na kanuni zake na kuhakikisha inatolewa kwa makandarasi wa ndani hususani katika miradi inayotekelezwa kwa kutumia fedha za ndani ambapo amewakumbusha makandarasi kuwa na weledi pamoja na maadili katika utekelezaji wa miradi ili kufanikisha miradi hiyo inapomalizika iwe inalinganana thamani ya fedha iliyotumika. 


Aliongeza kwa kuwataka makandaradi hao kuepunda vitendo vya rushwa ambavyo vinaweza kupalekea kutokukamilika kwa wakati na kwa ubora miradi wanayope kuisimamia huku akiipongeza bodi hiyo kwa kuboresha mifuko ya kusaidia makansarasi wote wa ndani bila kujali daraja la kusajili.


Awali msajili wa bodi ya makandarasi Injinia Rhoben Nkori alieleza katika mwaka 2020 bodi hiyo imesajili makandarasi 907 ambapo sasa hivi bodi hiyo ina makandarasi 11749 na kusajili miradi ya ujenzi 3179 yenye thamani ya trilioni 3.8,katika miradi hiyo asilimia 96.7 yenye thamani ya asilimia 46.5 ilifanywa na makandarasi wa ndani huku miradi yenye thamani ya asilimia 23.5 ilifanywa na wakandarasi wa kigeni.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi hiyo Consolata Ngimbwa alisema  amewataka makandarasi hao kuwa na umoja utakao wasaidia kuwasilisha hoja zao huku wakiepuka kuwa na vikundi ambavyo mwisho wa siku vikundi hivyo haviwezi kutatua changamoto zao.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: