Na Heri Shaaban (ILALA)
MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam Omary Kumbilamoto amewapongeza Watendaji ,Wakuu wa Idara na madiwani kwa kupata hati safi miaka sita mfurulizo.
Meya Kumbilamoto aliyasema hayo Dar es salaam jana wakati alipoandaa futari katika mfungo wa Ramadhani ambayo amewafuturisha wakazi wa Dar es salaam , madiwani wa Halmashauri ya Jiji na wafanyakazi wa Jiji.
"Ninawapongeza madiwani wangu kwa usimamizi wa miradi vizuri pamoja na Watendaji wa Halimashauri ya Jiji awali (ILALA )kwa usimamizi mzuri wa miradi kupelekea kupata hati safi kwa kipindi cha miaka sita mfurulizo " alisema Kumbilamoto.
Aliaema hati safi wameanzia kupata 2014/2015/2016, /2017, /2018, /2019, /2020 yote hiyo kutoka na kazi nzuri ambayo inafanywa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji na Watendaji wake.
Aliwataka Watendaji wa halmashauri ya Jiji hilo madiwani kushirikiana kufanya kazi ili kuisaidia Serikali ifikie malengo yake katika kujenga TANZANIA ya uchumi wa viwanda.
Aliwataka wakazi wa Dar es salaam kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassani katika kuchapa kazi
Aidha aliwapongeza Benki ya CRDB kwa ushirikiano wao mzuri ndani ya halmashauri hiyo ya Jiji kuunga mkono Juhudi, za Serikali sekta ya Elimu pamoja na kuleta maendeleo.
Post A Comment: